Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Havard nchini
Marekani, umegundua kwamba watu wanaopenda kula nyama kila siku wako
hatarini kupatwa na saratani ya utumbo kuliko wale wanaokula mara moja
moja.
Pia baadhi ya mafuta ya wanyama na yale yanayowekwa kwenye ‘baga’ au ‘cheese’ huweza kusababisha kansa.
Pia baadhi ya mafuta ya wanyama na yale yanayowekwa kwenye ‘baga’ au ‘cheese’ huweza kusababisha kansa.
Vile vile ulaji wa vyakula vilivyotengenezwa kwa
kuchanganya na nyama zilizosindikwa au kuhifadhiwa kwa matumizi ya muda
mrefu husababisha saratani pia.
Vyakula hivyo ni pamoja na ‘soseji’ ambazo hupendwa na
watu wengi. Pia mikate ya nyama ‘hot dogs’ nayo ni chanzo cha magonjwa
ya saratani.