Mimba inapotungwa, mwili huanza kupata mabadiliko ambayo huashiria ujauzito. Mabadiliko haya ndio msingi wa dalili za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, dalili hizi zinaweza zisiwe za wazi au zikatokana na magonjwa ya uzazi. Hapa ndio umuhimu wa vipimo vya mimba unakuja, kwani huwezesha kuthibitisha uwepo wa ujauzito.
Vipimo vifuatavyo hutumika kupima ujauzito:
- Kipimo cha Ujauzito cha Mkojo
- Kipimo cha Ultrasound
- Kipimo cha Ujauzito cha Damu
Kipimo cha Ujauzito cha Mkojo
Kipimo hiki hujulikana kama Urinary Pregnancy Test (UPT) kwa kiingereza. Ni njia ambayo hutumika sana kupima ujauzito. Hupima ujauzito kwa kutumia homoni inayoitwa human chorionic gonadotropin (hcg). Huweza kupima mimba kuanzia siku 8 -11 toka mimba kutengenezwa, au kuanzia tarehe aliyokuwa anategemea kupata siku zake.
Namna ya Kupima
Kusanya mkojo kwenye chombo safi, hasa ule wa asubuhi. Kisha dumbukiza kipimo mpaka kwenye mstari kwa dakika 1 halafu kitoe. Tazama mabadiliko ndani ya dakika 1-5 ikitegemea na maelekezo husika ya kipimo. Mstari mmoja ukibadilika hakuna mimba. Mistari miwili ikibadilika, ina maana kuna ujauzito. Kama hakuna mstari uliobadilika, kipimo hakifanyi kazi.

Kipimo cha Ultrasound
Ultrasound hutumia mawimbi ya sauti kupima ujauzito tumboni mwa mama . Kinaweza kupima mimba ya kuanzia wiki 4 – 6 na kuendelea. Kipimo hiki kinaweza kuonesha umri wa mimba, ukuaji wa mtoto tumboni na maendeleo yake. Kadri mimba inavyokua, huweza kutumika kujua jinsia ya mtoto. Ultrasound haina madhara yoyote kwa mama na mtoto.
Kipimo cha Ujauzito cha Damu
Kipimo hiki hupima homoni ya hcg kwenye damu. Ni njia yenye ufanisi mzuri ingawa haitumiki mara kwa mara.