Tatizo la mimba kutoka mara kwa mara ni tatizo ambalo huwatokea baadhi ya kinamama pale wanaposhika ujauzito.

Kitaalam tatizo hili hujulikana kama ‘ recurrent pregnancy loss’ uwezekano wa tatizo hili kutokea huongezeka kadri umri wa mwanamke unavyoongezeka.

Kuna sababu mbalimbali za mimba kutoka mara kwa mara, hizi zifuatazo:
  • Viuvimbe vya mji wa uzazi (uterine fibroids)
  • Kushikana kwa kuta za mji wa mimba.
  • Matatizo ya mji wa mimba ya kuzaliwa nayo (congenital malformation). Kizazi huwa hakina umbo au nafasi ya kutosha kuruhusu mtoto akue mpaka kuzaliwa.

  • Shingo ya Uzazi kulegea (cervical incompetence). Kadri mimba inavyokua, shingo ya uzazi hushindwa kuhimili na hivyo mimba hutoka.
  • Vichochezi kutokaa vizuri (hormonal imbalance)
Pamoja na hayo, kuna dalili za tatizo hili la mimba kuharibika mara kwa mara na miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na kutokwa kwa damu ukeni, maumivu ya tumbo hasa chini ya kitovu na kiuno, kutoa uchafu au sehemu ya mimba iliyoharibika.
 
Top