Utandu mweupe(oral thrush) unakuwa kama maziwa kwenye kinywa cha mtoto ni infection inasababishwa na fungus wanaoitwa candida albicans.
Utandu(thrush) huo unamwadhiri mtoto sehemu ya ulimi ,kuta za mashavu kwa ndani na ufizi linawapata haswa watoto wachanga waliotoka kuzaliwa mpaka miezi 2-4,pia inawapata watoto wakubwa na watu wazima pia.
Sababu ya mtoto kupata utandu kinywani ni nini?
Candida fungus wanapoongeka kuwa wengi mwilini ndio wanasababisha mtoto kupata utandu kinywaji.candida fungus nao wanasababisha na haya matatizo ndio wanakuja kuzalishwa wengi kwenye mwili wa mtoto
Hana kinga ya kutosha mwilini na bado inajitengeneza ndio hapo inakuwa rahisi kwake kupata infection.
Mama alivyokuwa mjamzito au mtoto anapotumia dawa za antibiotic anapunguza kinga ya mwili ndio mana inakuwa rahisi kushambuliwa.
Mtoto akitumia antibiotic inasababisha kupunguza kinga wa bacteria
Mama anaenyonyesha nae akitumia antibiotic inachangia mtoto kupata utando
Mtoto anaweza pata hili tatizo kipindi anapozaliwa kupitia uke wa mama
Dalili za utando (thrush)
Mtoto atalia wakati wa kunyonya au kula
Mtoto atapata vipele vidogo vidogo sehemu ya matako,mapajani (diaper rash)
Utandu mweupe usio futika hata ukifutwa sehemu za ufizi juu,kuta za mashavu na juu ya ulimi
4.Utando unaweza ambatana na rangi nyekundu kama damu kwa mbali
5.Kunuka mdomo wa mtoto
Tiba
Utajuaje kama ni utando wa maziwa au infection? ,safisha mikono yako vizuri kwa maji safi na sabuni,jaribu kuifuta na kidole uone kama inaweza toka ,iwapo ikatoa ujue hayo ni maziwa tu ndio yametengeneza utandu,isipo toka ujue ni infection.
Utandu huo unaweza mletea mtoto vidonda pia mdomo ,utajua wakati wa kunyonyesha au kumpa kuchupa ya chuchu kunyoa anashindwa na kulia kutokana na maumivu anayopata,mpeleke hospital watamwandikia dawa ya maji au gel atakayo tumia baada ya wiki 1 hapo utaona mabadiliko.Madhara ya utando wa kiunywa unaweza mletea mtoto nappy rash
Homeremedies-tiba asilia unayoweza itengeneza nyumbani tumia
Mafuta ya nazi mpake sehemu ilio adhirika na mama paka kwenye chuchu,nazi ina fatty acid inasaidia kuuwa fungus, na inauwezo wa kurudisha kinga.
Apple cider vinegar nayo unaweza mpaka haina madhara
Mama anaweza kunywa mtindi (yoghut) inasaidia ila usimpe mtoto chini ya miezi 6-7
Baking soda -chemsha maji kikombe yakishachemka kabsa,epua na kuacha ya poe kidogo yawe vugu vugu kwa mbali weka baking soda koroga chukua kitambaa safi lowesha hayo maji na mpangusie mtoto kinywani penye utando.
Ushauri
Usafi ni muhimu sana kwa mtoto,mama hakikisha matiti yako unasafisha vizuri sehemu ya chuchu kabla ujamnyonyesha ili tatizo lisijirudie sababu infection inaweza hamia kwenye chuchu,hakikisha unaosha vizuri chupa zake au pacifier (chuchu ya plastik) kama mnampa kuinyonya.
Unaweza mpa paracetamol kupunguza maumivu ili amudu kula chakula (maziwa).Mama anae nyonyesha au mjamzito acha kutumia antibiotic inapunguza kinga ya mtoto na yakwako pia, sio kila ugonjwa lazima utumie antibiotic ni kali sana.