imageMaziwa ya mama ni muhimu sana kwa mtoto ,yanampa lishe na afya nzuri .Maziwa ya mama  yana virutubisho,calories na vimiminika vya kutosha.

image



FAIDA YA MAZIWA YA MAMA.
Mwongezea uzito kwa haraka.

Yana mwepusha na maradhi mengi cancer,mzingo (allergy)

Anaepuka kupata infection ya masikio

Pumu

Inampa kinga ya kumwepusha kuhara mara kwa mara



       FAIDA YA MAMA KUNYONYESHA
Ni rahisi yanapatikana mda wowote sio gharama.

Mama anaponyenyesha anapùnguza hatari ya kupata cancer.

Inamsaidia kuchelewesha kuona hedhi ya mama na kumfanya kutunzwa kwa madini ya chuma mwilini.

Itakusaidia kuimarisha mifupa ukija kuzeeka .



    SABABU ZINAZOMFANYA MTOTO ASHINDWE KUNYONYA
Anamaumivu mdomoni (vidonda)mchunguze

Infections ya sikio(anapata maumivu makali anashindwa kuvuta maziwa)

Mama unatumia mafuta au perfume yenye harufu kali.

Utokaji wa maziwa umepungua hivyo atakuwa anatumia nguvu kunyonya na hayatoki .

Kuota kwa meno kunamsababishia mtoto kukataa kunyonya ,sababu fizi zinakuwa zinamvimba .

Mama unapokula vyakula kama kabichi,maharage,jibini(cheese),broccoli, au maziwa ya unga (NIDO) inamsababishia kumpa gesi tumboni na anaweza kataa kunyonya haswa kwa watoto wachanga miezi 0-6 hapo.



Mama ni muhimu  kumnyonyesha mtoto  ,acha kutumia maziwa ya kopo kama unauwezo wa kunyonyesha , kama wewe unafanya kazi basi pump(kamua)maziwa mwachie house gal atampa mtoto ,yahifadhi hayo maziwa kwenye friji!

Kwa watoto wanaopewa maziwa ya kopo(baby formula)iwapo ameyakataa inabidi umbadilishie .
 
Top