UTANGULIZI – YAJUE MAGONJWA YA MOYO

Magonjwa ya Moyo ni magonjwa yanayoambatana na kuathiri moyo. Mara nyingi magonjwa ya moyo yanaambatana na mishipa ya damu kuwa na tatizo ambapo moyo hushindwa kufanya kazi, moyo hutegemea damu ambayo hubeba oxygen, madini, vitamins, kinga ya mwili, joto, homoni na vingine vingi.

Kwa mwaka 2015 pekee zaidi ya watu milioni 17.7 walifariki kutokana na magonjwa ya moyo na mfumo wa damu. Hii ni sawa na theluthi ya vifo vyote duniani. Zaidi ya theluthi ya vifo vyote vinavyotokana na ugonjwa wa moyo na mishipa ya damu hutokea ndani ya nchi zenye uchumi wa chini na uchumi wa kati


Different-Problems-of-the-Heart.

AINA ZA MAGONJWA YA MOYO


Zipo aina mbalimbali za magonjwa ya moyo hutofautiana japo yote huathiri moyo, nayo ni;


Ugonjwa wa moyo unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu (Coronary artery disease) Hili ni tatizo linalowakuta watu wengi, mishipa ya damu hupasuka na kuharibika hii hutokana na mishipa ya damu kuwa na uchafu na mafuta mengi na kufanya damu isipite vizuri

Mapigo ya moyo kwenda tofauti (Heart Arrhythmias) Hii hutokea pale mapigo ya moyo kwenda taratibu isivyo kawaida au kwenda haraka isivyo kawaisda, pia mapigo ya moyo kwenda ovyo. Hii ni hatari sana na huua sana

Moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure) Hii ni hali moyo hushindwa kufanya kazi yake kama kupampu na kusambaza damu, kusambaza oxygen. Hii inaweza kutokea kwa mtu mwenye magonjwa kama ugonjwa wa moyo wa misipa kuathirika, Shinikizo la damu, na magonjwa mengine

Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa (Congenital heart disease) Haya ni magonjwa ambayo wengi huzaliwa nayo, yanaweza kuwa ni baadhi ya kasoro katika mwili kama baadhi ya chemba za moyo kuziba au kupasuka, oxygen kupita kwa shida na vinginevyo.

Ugonjwa wa valvu na misuli ya moyo (Heart Valve Disease & Cardiomyopathy (Heart Muscle Disease)) Katika moyo kuna chema nne nazo zinapitisha damu na  oxygen kutoka kwenye mapafu, valvu hufunguka na kufunga. Valvu na misuli ikiwa imepasuka na kuharibika husababisha tatizo la moyo.

Moyo kutanuka. Hii hutokea pale damu ikiingia ndani ya moyo harafu mishipa ya kutoa damu ikiwa na tatizo ikashindwa kutoa damu nje ya moyo moyo utaanza kutanuka siku hadi siku. Kutanuka kwa moyo kunatokea usipotibu baadhi ya matatizo kama shinikizo la damu, moyo kwenda mbio, valvu na misuli ya moyo n.k.

Shinikizo la damu (B.P) ni shinikizo la damu yako kwenye kuta za mishipa yako kwani moyo wako unasukuma karibu na mwili wako. Unaweza kuwa na shinikizo la damu (shinikizo la damu) kwa miaka bila dalili yoyote.

Mshtuko/ Shambulio la moyo (Heart Attack). Ni kifo cha sehemu ya misuli ya moyo inayosababishwa na kuzuiwa wa usambazaji wa damu. Amana zilizo na mafuta huunda kwa wakati, na kutengeneza alama katika mishipa ya moyo wakoIkiwa baadhi ya misuli ya moyo inakufa, mtu hupata maumivu ya kifua na kukosekana kwa umeme kwa tishu za misuli ya moyo.

Chembe ya Moyo. Hii ni maumivu ya upande wa moyo maeneo ya kifua hutokea wakati unafanya kazi au hata kama umekaa kama ni yenye kukubuhu. Maumivu haya huambatana na kutokwa jasho na kukosa hewa. Hutokana na moyo kukosa damu ya kutosha.

CHANZO CHA MAGONJWA YA MOYO


Magonjwa ya moyo hutokea pale ambapo moyo huathiriwa na kuharibiwa kwa vitenda kazi vyake. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata magonjwa ya moyo nayo ni pamoja na;


Heart-Disease

Kuwa na halemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P)

Kuvuta sigala

Uzito kupita kiasi na unene uliozidi

Kisukari

Kukaa sehemu kwa mda mrefu bila kuufanyisha kazi mwili

Umri

Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi

Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili

Historia magonjwa yanayoambatana na moyo katika familia

DALILI ZA UGONJWA WA MOYO


Mara nyingi dalili hujionesha wakati mtu kakaa na ugonjwa kwa mda mrefu kidogo, ila kuna zingine zinatangulia na mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia. Uonapo baadhi ya dalili fanya mawasiliano.


Moyo kwenda mbio (Moyo kudunda kwa nguvu isivyo kawaida )

Uchovu uliopitiliza, mwili kuwa dhaifu na kuchoka haraka hata kwenye shughuri ndogo

Maumivu ya kifua hasa yanayotembea mpaka kwenye mabega, shingo au taya

Kushindwa kulala vizuri hasa kushtuka usingizini kuhisi kama unakabwa na kukosa pumzi

Tumbo kujaa, kichefuchefu na kutapika

Kukosa pumzi au kushindwa kupumua vizuri hasa unapolala chali

Miguu, uso na tumbo kuvimba na kujaa maji

JINSI YA KUEPUKANA NA MAGONJWA YA MOYO


Fanya mazoezi – Angalau dakika 30 kwa siku

Usile vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi

Usitumie chumvi mbichi au chumvi nyingi

Punguza (balansi) kiwango cha halemu (choresterol)

Balansi usito wako

Usivute sigara

Punguza au acha kunywa pombe

Punguza mawazo

Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali

Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa 7 hadi 9

TIBA YA MAGONJWA YA MOYO

Magonjwa ya moyo yanatibika kwa hali tofauti, pia kufuatana na mda wa tatizo, mara nyingi wagonjwa wamekuwa wakikata tamaa na kuwa wabishi, hii hufanya wengi kufa kutokana na kuto kuwa makini na kile tunacho waeleza.

 
Top