Habari za Jumatatu ya Septemba, 14, 2015 mdau wa www.dkmandai.com bila shaka umzima wa afya tele.

Leo napenda kuzungumzia kuhusu mmea wa mparachichi hususani yale majani yake ambayo nayo yanauwezo wa kutibu shida mbalimbali ndani ya miili yetu.

Parachichi kama tunda tayari tumeshalizungumza sana, lakini leo napenda tugusie kuhusu majani ya mti wa mparachichi wenyewe.

Matumizi ya majani ya mparachichi yana nafasi kubwa ya kumsaidia mwanamke ambaye hupata maumivu wakati wa hedhi, kinachotakiwa kufanyika ni kupata majani 6 ya mparachichi kisha chemsha kwenye maji lita moja baada ya hapo yaache yapoe kisha tumia maji hayo kwa kunywa glasi moja asubuhi mchana na jioni utaona mafanikio.

Aidha, majani hayo pia husaidia sana kuongeza kiwango cha maziwa kwa kinamama, endapo mama atatafuna jani moja la parachichi kila siku, lakini hakikisha jani unalotafuna ni safi na umeliosha vizuri.

Pia majani haya ya mparachichi ni msaada sana katika kutibu majeraha, ili kufanikiwa katika hili unapaswa kusaga majani hayo kisha weka kwenye sehemu yenye jeraha na utaona mafanikio,

Majani ya mparachichi pia husaidia kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali na kumuepusha mhusika kukumbwa na vimelea vya magonjwa.
 
Top