Ni wakati mwingine tena tuKiendelea kufahamishana yale mambo muhimu yenye manufaa kwa afya zetu, na sasa ninayo furaha kukuletea  hizi njia za kuepukana na harufu mbaya ya kinywa.

Nimekuwa nikipokea maswali mengi kuhusu tatizo hili na wengi wakiomba msaada wa kufahamu njia za kufanya ili kuepukana na shida hii.

Tayari ninazo hapa hizo mbinu za kuepukana na shida hiyo unaweza kuzisoma hapa chini>>>

Kwanza kabisa ili kuepuka tatizo hili ni vyema kujitahidi kula matunda na mboga za majani pamoja na kunywa maji mengi kila siku, vyote hivyo husaidia sana kumaliza shida hiyo kwa sababu husaidia kinywa kuwa katika hali ya unyevunyevu muda wote.

Aidha, shida hii huweza kutibika kwa kutumia majani ya mwembe, ambapo mhusika atapaswa kutumia majani ya mwembe kwa kutafuna kila anapohisi hali ya kinywa kuwa na harufu mbaya au kila baada ya kupata mlo.

Majani mengine ambayo husaidia kumaliza tatizo hilo ni pamoja na majani ya mpera ambayo mhusika atapaswa kuyatumia kama ilivyo kwa majani ya muembe.

Pia unaweza kutumia mdalasini ili kumaliza tatizo hili, unachopaswa kufanya ni kuchemsha maji kwa dakika 5 kisha weka vijiko viwili vya unga wa mdalasini ndani ya kikombe chenye maji na usubiri yapoe baada ya hapo utakunywa hayo maji kila mara baada ya kupata mlo wako. 

Karafuu nayo husaidia sana kuondosha tatizo hili kwa kutafuna kila unapomaliza kupata mlo wako.

Lakini pia ili kuepukana na tatizo hili ni vyema kuepuka matumizi ya vyakula vyenye sukari nyingi ambavyo huweza kuwa na madhara kwa afya ya kinywa na meno. 
 
Top