Matatizo ya aina hii mara nyingi huwapata watu ambao shughuli zao huwalazimisha kutembea kwa muda mrefu, kusimama kwa muda mrefu au kukaa kwa muda mrefu wakati miguu ikiwa imening’inia.

Tabibu Abdallah Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic anasema kuwaka moto kwa miguu na nyayo husababishwa na mzunguko dhaifu wa damu katika miguu au ukosefu wa virutubisho na madini yanayohitajika mwilini.

Mtaalam huyo anabainisha kwamba, chakula cha asili kinahitajika zaidi ili kuondoa sumu zinazoleta athari hizi ndani ya mwili. Pamoja na kufanya mabadiliko katika aina ya vyakula vitakavyoliwa kwa ajili ya kupata virutubisho na madini muhimu.
 

Tabibu Mandai anaeleza baadhi ya tiba ambazo zinaweza kuondoa tatizo hilo kama ifuatavyo.

Limao 
kuhusu limao mtaalam huyo anasema mhusika anapaswa kuosha miguu na nyayo kwa maji ya moto na sabuni na baadaye kukata limao katika vipande viwili kisha kupaka sehemu zile ambazo huwa unahisi kama kuungua.

Maji ya uvuguvugu /chumvi. 
Wakati umekaa, tumbukiza miguu ndani ya maji ya uvuguvugu, yaliyoongezewa na chumvi ya mawe yakiwa ndani ya karai kwa muda wa nusu saa, lakini wakati umetumbukiza miguu unakuwa unaosha sehemu ambazo huwa unajihisi kuwaka moto.
 
Top