Kitunguu maji ni moja ya kiungo ambacho hutumika karibu kila siku katika mapishi ya kila siku, lakini kiungo hiki pia kina nafasi yake katika kutibu magonjwa mbalimbali.

Leo nimeona kuna haja ya kuzungumzia kiungo hiki ili kiweze kukupatia msaada katika kutibu magonjwa yanayokuandama, lakini pia kutumika kama kinga ya magonjwa mengine.

Matumizi ya kitunguu maji husaidia sana kuondosha dalili zote za magonjwa ya moyo ikiwa ni pamoja na ile hali ya kuziba kwa mishipa ya damu ya kwenye moyo, lakini pia vitunguu husaidia sana kumuepusha mhusika dhidi shinikizo la damu 'blood pressure' au mshituko wa moyo 'heart attack'

Kitunguu maji pia huweza kutumika kama kiongeza damu mwilini kutokana na kuwa na utajiri wa madini chuma ndani yake hivyo huweza kuwa ni msaada mzuri na muhimu kwa wenye anemia.

Kitunguu pia husaidia kuongeza uwezo wa kongosho kuzalisha insulin ya kutosha na hivyo kupelekea mwili kuwa katika kiwango cha sukari kinachohitajika mwilini.

Aidha, kitunguu pia kina sifa ya kutibu matatizo ya ngozi, kinachofanyika katika swala hili ni kutengeneza juisi ya kitunguu kisha paka sehemu iliyoathirika na utaona mafanikio.

Kwa wale kina dada wenye shida ya kukatika kwa nywele basi unapotumia juisi ya kitunguu maji husaidia sana kuondosha tatizo hilo na kuzifanya nywele kukua vizuri na kuonekana kuwa na afya nzuri. Kinachopaswa kufanyika katika hili ni kutumia juisi hiyo ya kitunguu maji na kupaka kwenye shina ya nywele kwa kila wiki mara mbili. Fanya hivyo kwa miezi kadhaa.

Pia kitunguu maji kinauwezo wa kupambana na vijidudu vinavyosababisha kifua kikuu TB pamoja na maambukizi kwenye njia ya mkojo yaani U.T.I
 
Top