Kauli ya mhariri: Wananchi walio na mapato ya kadiri wameacha kula vyakula vya kiasili ambavyo huwa vyenye afya. Wananchi hao wamegeukia vyakula ambavyo havisaidii chochote mwilini, ambavyo husababisha magonjwa. Kulingana na mtaalamu wa lishe, vyakula vilivyo na mafuta, sukari, chumvi nyingi na visivyo na nyuzi vimekubalika katika jamii kutokana na mapato yaliyoimarika na uigaji wa hali ya maisha kutoka ughaibuni.Vyakula hivyo ni vifuaavyo:
Vibanzi(Chips).
Viazi karai huwa na kiwango kikubwa cha mafuta na vitu vingine visivyo bora kwa mwili. Huwa vinasababisha uzito. Chumvi itiwayo vibanzi huwa hatari kwa watu walio na shinikizo la damu au wanaougua kisukari, au walio na miaka zaidi ya 5.
Chumvi husababisha madini mwilini kuweka maji mengi na kusababisha moyo kushindwa kupiga damu.
Hii ni aina ya nyama iliyowekwa kemikali ili kuifanya kukaa zaidi bila kuharibika. Nyama hii ni kama soseji, salami na aina zingine za nyama. Hizi aina za nyama zinahusishwa kansa, na magonjwa ya moyo.
Kuku aliyekaangwa kwa mafuta
Aina hii ya kuku huwa na mafuta mengi ambayo yanaweza kusababisha mafuta mengi mwilini na magonjwa ya moyo. Mafuta hayo huwa pia yanaweza kusababisha kansa kutokana na uzito mwingi.
Nyama Choma
Ladha ya moshi na nyama iliyoungua ni hatari sana kwa afya yako. Mafuta ya nyama na joto husababisha kemikali hatari zinazoweza kusababisha kansa na uchungu magotini. Kutokana na hali kwamba nyama choma huliwa kwa chumvi ambayo haijapikwa huongeza hatari ya kupatwa na shinikizo la damu.
Spaghetti-Noodles
Huwa zimetengenezwa na kemikali nyingi zilizo na uwezo wa kusababisha shinikizo la damu na ugonjwa wa figo.
Soda
Pombe