Kama binadamu wote duniani kote wanavyoishi kwa muda mrefu zaidi.Kwa karne iliyopita,umri wamaisha ya binadamu katika nchi nyingine umeongezeka hii ni kwa sababu ya kuongezeka kwa huduma za afya,mbinu nzuri za kilimo pamoja na kuzuia vifo vya watoto wadogo wakati wa kujifungua na wakati wa makuzi.
Hata hivyo licha ya kuwa Marekani ndiyo nchi yenye utajiri mkubwa zaidi duniani na watu wake wanaishi katika maisha ya juu kimaisha na wanajitosheleza kwa karibu kila kitu lakini cha kushangaza ni kwamba Marekani haimo katika nchi 10 zinazoongoza kwa kuwa na maisha marefu.Suara la Marekani linaangukia pia kwa Tanzania,licha ya kuwa na mazingira mazuri yasiyokuwa na kemikali na mambo ya hatari yanayoweza kupunguza afya.Lakini bado watanzania wameendelea kuwa katika kiwango cha chini cha maisha ya kuishi kwa wastani ambao huwa unatolewa na umoja wa mataifa kwa kila mwaka.
Hii yote inachangiwa kwa kiasi kikubwa sana na serikali ya Tanzania na watanzania wenyewe kutotilia mkazo zaidi katika masuala ya Afya ya mama na mtoto,katika kipindi hiki cha mabadiliko ya hewa.Ufinyu wa elimu kuhusu ulaji na mabadiliko ya tabia ya nchi kunakofanya watu waendelee kuwa katika ugumu wa maisha,ambako husababisha ulaji mbovu usiokidhi mahitaji muhimu ya mwili.
Ni jukumu sasa la serikali kuweza kutilia mkazo katika maswala ya afya pamoja na kuwapa watanzania elimu ya kutosha juu ya ulaji na namna bora ya kuishi kunakofata sheria na kanuni za afya.
Masahihisho ya makala hii yamefanywa August 2, 2016.
ZIFUATAZO NI NCHI HAPO HCHINI ZINAZOOGOZA KWA KUWA NA UMRI MREFU ZAIDI WA KUISHI KULIKO ZOTE DUNIANI.
NAMBA 10::ICE LAND
Wastani wa maisha kwa ujumla: 82
Wastani wa maisha kwa wanaume: 84
Wastani wa maisha kwa wanaume: 81
NAMBA9::ANDORA
Wastani wa maisha kwa ujumla: 82
NAMBA 8::JAPANI
Wastani wa maisha kwa ujumla: 83
Wastani wa maisha kwa wanawake: 87
Wastani wa maisha kwa wanaume: 80
NAMBA 7::SINGAPORI
Wastani wa maisha kwa ujumla: 83
Wastani wa maisha kwa wanawake: 86
Wastani wa maisha kwa wanaume: 80
NAMBA 6::SAN MARINO
Wastani wa maisha kwa ujumla: 83
Wastani wa maisha kwa wanawake: 86
Wastani wa maisha kwa wanaume: 80
NAMBA 5::HISPANIA
Wastani wa maisha kwa ujumla: 83
Wastani wa maisha kwa wanawake: 85Wastani wa maisha kwa wanaume: 80
NAMBA 4::ITALIA
Wastani wa maisha kwa ujumla: 83
Wastani wa maisha kwa wanawake: 85
Wastani wa maisha kwa wanaume: 80
NAMBA 3::USWIZI
Wastani wa maisha kwa ujumla: 83
Wastani wa maisha kwa wanawake: 85Wastani wa maisha kwa wanaume: 81
NAMBA 2::HONG KONG
Wastani wa maisha kwa ujumla: 84
Wastani wa maisha kwa wanawake: 87Wastani wa maisha kwa wanaume: 81
NAMBA 1::MONACO
Wastani wa maisha kwa ujumla: 89