Saratani ya shingo ya uzazi ni saratani inayoongoza kwa vifo na ugonjwa unaotokana na saratani hapa duniani na Tanzania. Saratani hii inaweza kutibika iwapo itagunguliwa mapema kwa kufanyiwa uchunguzi. Hutokea mara nyingi kwa wanawake wenye umri wa
zaidi ya miaka 30.
Chanzo cha Saratani ya Shingo ya Uzazi
Saratani ya shingo ya uzazi hutokea kutokana na mabadiliko ya seli katika shingo ya uzazi ambayo husababishwa na aina ya kirusi kinachoitwa Human Papilloma Virus (HPV). Kirusi hiki huambukizwa kwa njia ya kujaamiana na mtu mwenye maambukizi ya kirusi cha HPV.
Dalili
Saratani ya shingo ya uzazi huanza na kuendelea kwa muda mrefu bila kuonesha dalili zozote. Dalili zinaweza kujitokeza wakati ugonjwa upo katika hatua za mwisho.
Chanzo cha Saratani ya Shingo ya Uzazi
Saratani ya shingo ya uzazi hutokea kutokana na mabadiliko ya seli katika shingo ya uzazi ambayo husababishwa na aina ya kirusi kinachoitwa Human Papilloma Virus (HPV). Kirusi hiki huambukizwa kwa njia ya kujaamiana na mtu mwenye maambukizi ya kirusi cha HPV.
Dalili
Saratani ya shingo ya uzazi huanza na kuendelea kwa muda mrefu bila kuonesha dalili zozote. Dalili zinaweza kujitokeza wakati ugonjwa upo katika hatua za mwisho.
Kutokwa na damu isiyo ya hedhi ukeni.
Damu hii inaweza ikatoka katika hali zifuatazo;
- Kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana.
- Kutokwa na damu ukeni kwa wanawake waliokwisha kukoma hedhi.
- Damu iliyochanganyikana na majimaji ya uke
- Matone ya damu au damu kutoka kipndi kisicho cha hedhi.
Inaweza kuwa ni kutokwa na maji yenye harufu mbaya ukeni, kutokwa na usaha ukeni au maji maji ya ukeni mengi yenye damu damu wakati mwingine.
Maumivu wakati wa kujamiiana
Dalili nyingine zinazoweza kutokea ni maumivu ya kiuno, kukojoa mkojo wenye damu, kupitisha mkojo na haja kubwa kwenye uke na upungufu wa damu.
Tabia Hatarishi Kupata Saratani ya Shingo ya Uzazi
Tabia zifuatazo huongeza hatari ya mwanamke kupata saratani hii:
Kuanza ngono mapema katika umri mdogo (chini ya miaka 18).Kuwa na wapenzi wengi au kuwa na mpenzi mwenye wapenzi wengi (huleta urahisi wa kupata virusi vya Human Papilloma Virus)
Uvutaji wa sigara
Kuzaa watoto wengi
Upungufu wa kinga mwilini
Kugundua Saratani ya Shingo ya Uzazi
Saratani ya shingo ya uzazi huchukua muda mrefu mpaka kuonesha dalili, na hivyo ugonjwa kuwa umefika hatua za mwisho pale dalili zinapojitokeza.
Kipimo cha uchunguzi kinachafanyika huitwa Papanicolaou Smear (Pap smear), inashauriwa kufanya kipimo hiki angalau mara moja kwa mwaka kwa wanawake wenye miaka 21 na wanashiriki ngono.
Matibabu
Matibabu ya saratani hutolewa kutokana na hatua ya ugonjwa. Hatua za mwanzo za ugonjwa huweza kutibika kabisa (ingawa kuna uwezekano wa kujirudia) na hatua za mwisho za ugonjwa huu huwa haziwezi kupona kabisa. kinachofanyika mara nyingi ni kutoa matibabu yatayotuliza dalili na maumivu na kumuwezesha mgonjwa kuishi vizuri. Huduma za matibabu hutolewa kwa njia zifuatazo:
Upasuaji katika hatua za mwanzo za ugonjwa.Mionzi.
Dawa za Saratani.
Mionzi pamoja na dawa za saratani.
Namna ya Kujikinga au Kuzuia Saratani ya Shingo ya Uzazi
Kupata chanjo ya Human Papilloma Virus.Kuepuka ngono katika umri mdogo.
Kuwa na mwenzi mmoja mwaminifu.
Kutumia kondomu kila mara unapojamiiana.
Epuka kuvuta sigara.
Kufanyiwa uchunguzi wa ya shingo ya kizazi angalu mara moja kwa mwaka.