Ugonjwa wa moyo ni yale magonjwa ambayo huathiri moyo na mishipa yake, lakini hapa nimeona ni vyema tufahamishane hizi dalili za tatizo hili.
 

Kwa kawaida huwa hakuna dalili inayojitokeza mpaka pale moyo unaposhindwa kufanya kazi ghafla (heart attack), au mtu anapopata kiharusi.

Hata hivyo, dalili za ugonjwa wa moyo hutofautiana kutegemeana na aina ya ugonjwa wa moyo, miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na hizi zifuatazo:

  • Kujihisi kuchoka na kuwa dhaifu.
  • Maumivu ya kifua (hii ni dalili kuu ya ugonjwa wa moyo)
  •  Maumivu ya mgongo, mabega, shingo na taya.
  •  Kukosa usingizi na wakati mwingine kupoteza fahamu.
  •  Kuvimba miguu, tumbo na mishipa ya shingo hujitokeza
Mambo ya kufanya ili kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo
  • Punguza  kula vyakula vyenye mafuta mengi  mara kwa mara
  • Epika ulaji wa nyama, hususani nyama nyekundu
  • Jitahidi kutumia nafaka hasa zile kama unga wa dona, jamii ya kunde, mbogamboga na matunda.
  • Fanya mazoezi ya mwili angalau dakika 30 kwa siku
  • Dhibiti uzito wa mwili
  • Hakikisha unaepuka msongo wa mawazo
  • Epuka uvutaji wa sigara au utumiaji wa tumbaku
Ni vyema ikafahamika kwamba hadi mtu kuanza kupata dalili hizi basi amekuwa tayari ameishi na ugonjwa huo kwa muda mrefu. Hivyo, njia bora ya kugundua mapema dalili ya ugonjwa /magonjwa kujenga utaratibu wa kuchunguzwa afya yako mara kwa mara. 
 
Top