Maana ya Shinikizo kubwa la Damu: Ni ongezeko la nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa inayochukua damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye viungo na tishu mbalimbali mwilini.

Ukubwa wa shinikizo hilo la damu utegemea wingi na nguvu ya msukumo wa damu kutoka kwenye moyo na ukubwa wa mishipa inayopeleka damu mwilini.


Kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu mwilini ni 120/80mmHg au chini yake. Pale kiwango kinapokuwa 140/90mmHg au zaidi hali hiyo huwa ni shinikizo kubwa la damu

 Zifuatazo ni baadhi ya dalili za shinikizo la damu

  • Ukaumwa kichwa mara kwa mara hasa sehemu ya kisogo
  • Kutokwa na damu puani
  • Ukapata kizunguzungu
  • Kupata maumivu ya kifua
  • Moyo kwenda kasi wakati umepumzika
  • Kushindwa kufanya mazoezi kwa kushindwa kupumua
  • Kusikia mapigo ya moyo wako wakati umepumzika
  • Na kupata uchovu wa mara kwa mara.

Kwa bahati mbaya watu wengi huishi na tatizo hili kwa muda mrefu bila kufahamu kwani hakuna dalili zilizo bayana. Mara nyingi shinikizo kubwa la damu hutambulika pale unapokwenda kituo cha huduma ya afya kupima afya yako au kupata matibabu ya tatizo jingine la kiafya. Hali hii humweka mtu katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo hivyo ni muhimu kuwa na tabia ya kupima afya yako mara kwa mara.
 
Top