Unatafuta chakula kizuri cha kukuvutia kwa ajili ya kulala usingizi mzuri? Usitafute mbali, Ndizi ziko kila mahali unapopita , kwenye magenge, sokoni, na supermarket

Unashangaa? Hata mimi nilishangaa pia.

Nilipokuwa nataka kula Ndizi kawaida nilikuwa nakula asubuhi tu kwa ajili ya kuongezea breakfast yangu iwe na uzito , lakini mbinu ya kula ndizi usiku, saa moja au mawili kabla ya kwenda kulala ili chakula kiyeyuke vizuri tumboni. Virutubisho vya ndizi vinasaidia kuleta usingizi murua na kupata ndoto nzuri . hii ni moja ya hatua muhimu ya kulala , na husafisha vitu vyote ulivyokusanya tumboni kwa siku nzima.

 Sasa kwa nini basi ndizi zinakusaidia kufika kwenye ZZZ’S?

1.Zina Magnesium Ya Kutosha.
Watu wengi wamepungukiwa na magnesium na hata hawajui kuwa wamepungukiwa. Nashauri kabisa kwenda kwa dactari wako kupima kiasi cha magnesium ulichonacho. Dalili za kawaida kujua kama umepungukiwa na magnesium ni kuwa maumivu ya miguu wakati wa usiku, digestion yako kwenda polepole, na kutokupata usingizi mzuri, unakuwa unahangaika kutafuta usingizi kwa dawa. Lakini usiogope, Ndizi zipo na zina full magnesium kuliko hata matunda mengine.
Vyanzo vingine vya kupatikana kwa magnesium ni kula mbegu za maboga, na karanga.

2.Zina Potassium Ya Kutosha. 
Hiki chakula cha nguvu na kinachopatikana kwa urahisi kina virutubisho vingi tunavyohitaji .potasium inakamilisha magnesium ili kuboresha kupata usingizi mzuri na kusaidia digestion pamoja na kurahisisha msukumo wa damu.msukumo wa damu yako kwa kawaida unatakiwa uwe wa kawaida hata usiku , na hii ni dalili ya kuwa na afya ya moyo. Ukiwa na kiasi cha chini cha potassium inaweza kuchangia maumivu ya misuli na moyo kutokuwa na msukumo mzuri. Vyanzo vingine vya vinatokana na parachichi, broccoli na uyoga.

3.Zinaweza Kusaidia Kiasi Cha Amino Acid.
Amino acid na ikiwa ni mtangulizi wa serotonin na melatonin, (maneno ya kitaalamu haya) – vyote vina umuhimu kwa afya ya usingizi wa usiku.Serotonin inarekebisha na kudhibiti hali yako , wakati melatonin inarekebisha sikadiani ya mfuatano wa mwendo. , inayoshawishi, inayoshawishi homoni tunazotoa kila siku mchana na za usiku.
Vyanzo vingine vya Amino Acid ni pamoja na chia seeds, viazi vitamu, almonds, na majani ya kijani kabisa , kama spinachi.
 
Top