Ufwatao ni mwenendo wa maisha ambao una athari kubwa kwa ujauzito wako;

1. Kunywa Pombe
Mwanamke mjamzito hapaswi kunywa pombe. Unywaji wa pombe kwa mjamzito husababisha mjamzito kujifungua kabla ya muda, kuzaa watoto njiti (low birth weight babies), kuharibu mfumo wa ubongo au ufikiri wa mtoto na kuharibu mfumo wa viungo vya mwili vya mtoto.


2. Kuzidisha kunywa vinywaji vya chai, Kahawa, Energy na vyakula vya Chokoleti (chocolate)
Vinywaji vya Chai, kahawa, Energy na vyakula vya Chokoleti vina kilevi aina ya Caffeine, Utafiti wa kisayansi unasema kwamba kuzidisha sana kilevi cha Caffeine wakati wa ujauzito unaongeza uwezekano mkubwa wa kuharibu ujauzito (miscarriage). Kwa hiyo inatakiwa mjamzito apunguze matumizi ya vyakula hivi ili kunusuru ujauzito wake. Inatakiwa mjamzito anywe si zaidi ya kikombe kimoja cha chai au kahawa kwa siku, pia kwa upande wa vinywaji vya Energy inatakiwa mjamzito anywe si zaidi ya mls 250 kwa siku.

 Picha: Chai ya rangi

 Picha: Kahawa

Picha: Keki ya Chokoleti

3. Kula vyakula vya kupunguza uzito
Mjamzito hapaswi kula vyakula vya kupunguza uzito, kwani ulaji wa vyakula hivyo hata kwa muda mfupi huleta athari kubwa kwa mtoto wako alie tumboni. Mjamzito pamoja na mtoto aliyetumboni wanahitaji muendelezo wa virutubisho mbalimbali wakati wote wa ujauzito na baada ya kujifungua. Kama nilivyokwisha kueleza kwenye makala ya kwanza kuhusiana na Lishe kwa wajawazito, nilieleza kwamba Ongezeko la uzito kwa mjamzito ni kiashiria tosha kinachoonyesha kwamba ujauzito una afya njema. Ingawaje kwa upande mwingine vyakula vya kupunguza uzito havina virutubisho muhimu vinavyotakiwa katika ukuaji na maendeleo ya mtoto aliyetumboni. Ongezeko la uzito kwa mjamzito ni ishara ya ujauzito wenye afya njema, kwa hiyo mjamzito asithubutu kupunguza uzito. Kusoma makala ya kwanza kuhusu "Lishe bora kwa wajawazito" Bofya hapa

 Picha: Hivi ni baadhi tu ya vyakula vya kupunguza uzito, vitamfanya mjamzito ajisikie ameshiba wakati virutubisho vilivyopo ni kidogo sana vina uwingi wa maji, nyuzinyuzi (fiber) nyingi na vitamini ambazo bado hazitoshi kwa ukuaji wa mtoto. Hivi ni vyakula vya ziada kwa mjamzito.

Picha: Hivi ni baadhi tu ya vyakula vya kupunguza uzito, vitamfanya mjamzito ajisikie ameshiba wakati virutubisho vilivyopo ni kidogo sana vina uwingi wa maji, nyuzinyuzi (fiber) nyingi na vitamini ambazo bado hazitoshi kwa ukuaji wa mtoto. Hivi ni vyakula vya ziada kwa mjamzito.

4. Kutumia dawa za matibabu pasipo kuruhusiwa na wataalamu wa afya.
Mjamzito haruhusiwi kutumia dawa zozote zile za matibabu pasipo kuruhusiwa na daktari, Kwa sababu dawa hizo huweza kuleta shida kwenye ujauzito ikiwa ni pamoja na kutoa ujauzito, shida ya kujifungua na madhara kwa mtoto aliyetumboni.
Photo Credit: www.tervepotilas.fi

5. Kutumia madawa ya kulevya
Mjamzito haruhusiwi kutumia madawa ya kulevya ya aina yoyote ile kama Unga (Cocaine, Heroine na nyinginezo) na bangi. Madawa hayo hupita kwa urahisi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, na kuathiri ukuaji wa mtoto, vilevile dawa hizo husababisha mjamzito kujifungua kabla ya muda, kujifungua watoto njiti, mtoto kufia tumboni, watoto kufariki ghafra baada ya kuzaliwa kuanzia siku 0 hadi miezi 6 pia hadi kufikia miaka miwili.

Picha: Dawa za kulevya aina Cocaine /Heroin   Photo Credit: www.patch.com

6. Kuvuta sigara au bidhaa zingine za Tumbaku au kutafuna Tumbaku
Uvutaji wa sigara au bidhaa zingine za tumbaku au kutafuna Tumbaku ni hatari sana kwa afya ya mjamzito pamoja na mtoto, kwa hiyo mjamzito haruhusiwi kutumia bidhaa hizo. Moshi wa sigara huzuia damu isifike kwa mtoto kwa hali hiyo huzuia hewa safi ya Oksijeni, virutubisho kufika kwa mtoto pia huzuia uchafu kutoka kwa mtoto kwenda nje ya mfuko wa mtoto. Hali hii huweza kusababisha kifo cha mtoto akiwa tumboni. Vilevile uvutaji wa sigara husababisha kuzaliwa watoto njiti, pia huharibu mfumo wa ukuaji wa mapafu ya mtoto na huongeza atari ya kusababisha madhara ya mfumo wa upumuaji na kupata ugonjwa wa pumu kwa mtoto (Asthma) mara atakapozaliwa.

 
Top