Kumaliza mapema (Premature ejaculation) wakati wa tendo la ndoa ni tatizo linalowakumba wanaume wengi hivi sasa, Ingawaje dawa za aina mbalimbali zimekua zikitumika kutibu tatizo hili imeonekana kwamba bado tatizo hili linazidi kuongezeka kila kukicha. Tatizo hili limekua likichangiwa na mambo mengi sana, ikiwemo yafuatayo;
Mwenendo wa maisha wa hivi sasa yaani watu wengi wanakula vyakula visivyokua na virutubisho kamili.
Matatizo ya kiafya ya muhusika
Na sababu nyinginezo nyingi
Kama nivyokwishakusema hapo mwanzo kwamba sababu za tatizo hili ziko nyingi sana, hivyo basi inatakiwa tusuruhishe swala hili kwa kutibu mzizi wa tatizo. 

Mbali na sababu za kiafya na zinginezo Mfumo wa uzazi wa mwanamume una misuli ya uume iliyoanzia eneo la mifupa ya kiuno (Pelvic bone), misuli hiyo ndiyo kiini cha tatizo hili (Kumaliza mapema). Nikupe mfano mmoja; Chukua picha ya watu wanaoinua vitu vizito, watu hawa wanaongeza ukubwa wa misuli yao kwa kufanya mazoezi ya viungo. Je, unaweza kuongeza ukubwa na ukakamavu wa misuli kwa kunywa dawa?? Lahasha ni jambo lisilowezekana, bali kwa kufanya mazoezi ya viungo.

Kwa kutumia mfano wa hapo juu nikurudishe kwenye kipengele cha misuli ya uume, Misuli ya uume haina tofauti na misuli mingine ya mwili, mfumo wake ni uleule. Tatizo la wanaume wengi kumaliza mapema inasababishwa na kusinyaa kwa misuli hiyo (Pelvic muscle). Tazama picha hapo chini inayoonyesha misuli hiyo;


Picha: Kwa hisani ya mtandao

Misuli ya uume ikiimalika Mwanaume hamalizi mapema pia anakua na uwezo wa kusimamisha vizuri uume wake na unakua kakamavu sio legevu.

JINSI YA KUITAMBUA MISULI YA UUME (PELVIC FLOOR MUSCLE)
Misuli hii ya uume (Pelvic floor muscle) ipo mwanzoni kabisa mwa shina la misuli ya uume. Namna ya kuitambua misuli hii fanya ifuatavyo;

Nikuulize swali moja kidogo, Umeshawahi kubana mkojo?? Pengine upo maeneo ya hafla, darasani, ofisini, mpirani, kwenye gari ama safarini au sehemu ambayo unataka usipitwe na mada inayozungumziwa. Katika mazingira haya watu wengi wanajikuta wakibana mkojo kwa muda Fulani ili wamalizie uhondo wa mada Fulani au tukio fuani pengine yupo safarini na anajitahidi abane mkojo ili akojoe atakapofika.

Au ukiwa unakojoa maeneo Fulani yasiyo rasmi, pengine wakapita maofisa polisi ama migambo unajikuta unakatisha mkojo, Hivyo basi ile hali ya kubana au kukatisha mkojo unatumia misuli hiyo ya uume (Pelvic muscle), ndio breki ya mkojo.

Misuli hii ya uume ipo chini ya maungo ya mapaja katikati ya korodani na sehemu ya haja kubwa, mara nyingi sehemu hii ukiguswa au kutomaswa kwa kidole utaona uume unashtuka. Uuume unashtuka Zaidi ukiwa umesimama. 

Ndio maana wale watu wanaoingiliwa kinyume cha maumbile (Mashoga) wanaharibiwa misuli hii baadae mtu huyu (Shoga) anakuwa hana uwezo wa kusimamisha uume. Hivyo basi misuli hii ina kazi kubwa sana ya kuimarisha ukakamavu wa uume wako.

Hivyo basi misuli hii (Pelvic floor muscle) ndiyo inayotakiwa ifanyiwe mazoezi, sehemu hii ikiwa kakamavu uume unasimama vizuri na utaacha kumaliza mapema (Premature ejaculation).


NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI YA MISULI YA UUME (PELVIC FLOOR MUSCLE EXERCISE/KEGEL EXERCISES)
Kama nilivyoeleza mwanzoni kwamba kiini cha mazoezi haya ni misuli ya uume, Hivyo ile hali ya kubana mkojo ndio zoezi lenyewe. Sio kwamba ubane mkojo, Lahasha inatakiwa uwe kama unabana mkojo wakati huna hamu ya kukojoa. Fanya hivyo kwa nguvu kwa sekunde 3 alafu utaachia, pia utafanya tena kwa sekunde 3, Vilevile utaachia tena afu utafanya tena. Unaweza kuendelea hadi sekunde 5, 10 na 30 kadiri utakavyokua unaweza. Fanya zoezi hili wakati wowote uupendao haijalishi uume umelala au umesimama, Pia ukifanya zoezi hili wakati uume wako umesimama itakua bora zaidi na misuri yako itakazika vizuri.

Uendelee na zoezi hilo mara nyingi kadri uwezavyo, ukizoea utaweza kufanya zoezi hili kwa muda mrefu zaidi na sehemu yoyote ukiwa unatembea, ukiwa umekaa, kwenye gari na sehemu yoyote ile. Uzuri wa zoezi hili unaweza kufanya sehemu yoyote pasipo watu kujua.


>>Matokeo ya zoezi hili yanaanza kuonekana baada ya wiki 2-3 inategemea na mtu mwenyewe. Ukishapata matokeo mazuri usiache uendelee tu iwe ni kama sehemu ya maisha yako. Kwa mfano watu wanonyenyua vitu vizito wanakuza misuli yao yaani wanakua mabaunsa lakini wakiacha mazoezi wanabadilika wanakua wazembe ama manyama uzembe. Vilevile kwa upande wa misuli ya uume, jitahidi kufanya mazoezi haya mara kwa mara ili kuikaza misuli ya uume wako. Kwa kuanzia unaweza kufanya mara 3 kwa siku, pindi ukizoea unaweza kufanya mara nyingi kadiri uwezavyo.

CHANZO: MTANDAO WA INTANETI


 
Top