Mtoto kunyonya Kidole ama Ulimi, nini Chanzo?
Watoto hupishana linapokuja suala la kunyonya. Kuna wale ambao hujenga tabia ya kujinyonya, iwe ni ulimi au kidole cha mkononi, ingawa kuna wale wachache mno ambao hunyonya hata kidole cha miguuni wanapokuwa wadogo. Mtoto hua anaanza kunyonya ulimi ama kidole ikiwa atakuwa hakupata maziwa ya kutosha, mara nyingine husababishwa na matatizo ya kihisia. Mtoto asipotosheka kila anaponyonya huanza tabia ya kunyonya kidole au ulimi.
Kunyonya kidole au ulimi, ni moja ya njia ya mtoto kujibembeleza au kujipooza kwa hitaji lake wakati huo. Hii husaidia kwa mtoto kujizaidia apunguze njaa, ajibembeleze na hata katika kujisikia salama. Mara nyingi mtoto ataacha kunyonya kidole akiwa na umri wa miaka 3-6 ingawa watoto wengine huendelea hadi ukubwani.
Inasemekana kuwa tabia hii huanza tumboni baada ya wiki kumi na tatu za ujauzito na uendelea mtoto anapozaliwa ingawa wazazi wengi hugundua pale mtoto anapofikisha umri wa miezi miwili mpaka mitatu.
Nini Faida za Kunyonya Kidole?
Baadhi ya watafiti hudai huimarisha kinga ya mwili. Watafiti hao wanadai unyonyaji wa dole gumba na ung’ataji wa kucha husaidia kuzuia baadhi ya matatizo ya mzio (allergy).
Nini Hasara za Kunyonya Kidole au Ulimi?
Kunyonya kidole sio hatari ikiwa mtoto ataacha kunyonya kidole kabla ya miaka5. Kama mtoto atashindwa kuacha kunyonya kidole mpaka baada ya miaka 5, kuna uwezekanao mkubwa wa meno yake kutojipanga vizuri, kuota yamebebana na kupata meno yanayo shindwa kung’atana.
Baadhi ya watu huamini kuwa mtoto anayenyonya kidole ama ulimi hupunguza uwezo wa kukazia fikra masomo na hivyo kuwa mjinga, jambo ambalo kitaalamu halijathibitika.
Hata hivyo mtoto anae nyonya kidole mara nyingi huaribu mdomo na kuathiri midomo (lips) kwa kuzilegeza tokana na uzito wa kidole chake kwenye midomo. Huku yule ambaye hunyonya ulimi huwa na changamoto ya kukua na tabia hiyo hadi ukubwani ukilinganisha na yule anaye nyonya mdomo. Hiyo ni kutokana na kutokujitambua ama kujiona kuwa yupo kunyonya hivyo kuwa vigumu kujiachisha mapema Pia mtoto hua ana chelewa kuwa na ufaham kutokana muda mwIngi hutumia kunyonya kidole.
Inasababisha meno kutojipanga vizuri kwenye fizi. Madaktari wa kinywa wamehusisha matatizo ya kuwa na meno yasiyo jipanga vizuri na kunyonya kidole hasa kidole gumba kwani meno husukumwa kwenda mbele au kujipanga vibaya na hivyo kuathiri muonekano wake.
Watoto wanaonyonya kidole mara kwa mara baada ya miaka 4 au 5 na kuendelea wana hatari ya kupata tatizo la mpangilio mbaya wa meno, muonekano mbaya wa sura na hata matatizo ya kuongea vizuri.
Mpangilio mbaya huweza kujirekebisha wenyewe iwapo mtoto ataacha kunyonya vidole ingawa tabia hii ikiendelea mtaalam wa meno (orthodontists) atahitajika kumrekebisha. Kutokana na kunyonya vidole mtoto atapata tatizo la matamshi,na viungo vta mdomo kama ulimi kutoka nje wakati wa kuongea.
Infant Sucking Finger
Nifanye Nini Kumzuia Mtoto Kuacha Kunyonya Kidole?
Inashauriwa pale unapotaka kumshawishi mtoto kuacha kunyonya kidogo, kutumia njia sahihi ya kuelewesha na kumbembeleza mtoto kuliko kutumia nguvu.
Inashauriwa kuwa usimfanye mtoto aache kunyonya kidole akiwa na umri chini ya miaka 4 au 5 isipokuwa tu pale utakapoona kuna tatizo linalojitokeza kwa sababu ya kunyonya kwake kidole au ikiwa mtoto ataanza ghafla baada ya miezi kumi na ikiambatana na kuvuta nywele.
Mama napaswa kula vyakula vyenye lishe vitakavyomsaidia kutengeneza maziwa ya kuosha kuweza kumnyonyesha mtoto kila wakati anapoanza tu kunyonya kidole.
Kumueleza mtoto kwa upole na kwa lugha nzuri na ikibidi kumuahidi zawadi nzuri pale atakapokubali kuacha tabia hiyo.
Unaweza kumpeleka mtoto shule kwani kunaweza kusababisha aone aibu na kuacha hasa pale atakapo taniwa na wenzake anaosoma na kucheza nao.
Ataacha mapema kama utamzuia kunyonya kwa njia mbadala kama kupaka pilipili vidole vyake ili akinyonya aone ukali.
Mpatie mtoto michezo ambayo itaufanya huo mkono anaonyonya wakati wote uwe na shughuli ya kufanya, kama vile acheze puzzle, achezee midoli ili mradi tu viganja vyake viwe na shughuli.
Pia, unaweza kumnunulia mtoto nyonyo za plastiki ili akianza tu kunyonya kidole unampa anyone hii itamfanya asizoee kunyonya kidole.
Wengine hutumia mipira ya mikono/viganja (gloves) kuwavalisha watoto na kumfanya ashindwe kunyonya vidle vyake.
Iwapo vyote vitashindikana basi mzazi au mlezi asisite kuwaona madaktari wa afya ya meno ya watoto au daktari yeyote wa meno aliyekaribu nae kwa msaada zaidi.