afyaKatika nchi zinazoendelea, kila siku madaktari hulazimika kutibu wagonjwa wengi, ambao mara nyingi hufika vituo vya kutolea huduma na kupanga foleni. Kazi ya udaktari ni ngumu na yenye kuchosha sana hasa kukiwa na wagonjwa wasio na ushirikiano.

Mambo ambayo wagonjwa hufanya na kuwachukiza madaktari ni yapi?

Kuongopa. Kwanini wagonjwa huwadanganya madaktari? Kimsingi watu wote tuna siri ambazo tusingependa kumwambia mwingine, lakini unapofika kwa daktari unapaswa kuwa mkweli na kutoa habari zote zinazohusu unachoumwa kutia ndani mwenendo wako kingono, matumizi ya dawa zakulevya na tabia zingine mbaya.

Watu wengine huongopa kwa kuogopa baadhi ya matibabu kama upasuaji na kudungwa sindano. Watu wengi hawatambui kwamba kutotoa taarifa za kutosha kwa daktari kutafanya daktari kushindwa kutoa bainisho sahihi ya kile unachoumwa ili aweze kukuandikia matibabu sahihi yatakayo kuponya haraka.

Kujitolea bainisho la ugonjwa mwenyewe (Kujitibu). Kutokana na maendeleo ya kigitali kuwekuwepo na mitandao mbalimbali hasa ya intaneti kutia ndani wavuti tofautitofauti zinazorahisisha watu kupata hbari za magonjwa mbalimbali kutokana na dalili walizonazo.

Ingawa vyanzo hivi vinaweza kuwasaidia watu kutambua magonjwa yanayowasumbua ila yanaweza kuwa hatari ikiwa wagonjwa watajaribu kujitibu bila kumuona daktari. Wagonjwa waliosoma kwenye mitandao kwa muda mfupi habari kuhusu wanachoumwa huwalazimisha madaktari kutoa matibabu kulingana na walivyosoma na kuwafanya madaktari wakasirike sana.

Baadhi ya madaktari huuliza kwa ukali kwanini umekuja hospitali ikiwa unaweza kujitibu mwenyewe? Madaktari husoma na kujifunza kutibu kwa miaka mingi sana na hupata nafasi ya kuonana nawagonjwa wengi hivyo kusoma habari kwa dakika chache kwenye mitandao hakukufanyi kuwa daktari mzuri na kuweza kujitibu. Ni vyema kutambua ni daktari pekee anayeweza kutoa bainisho sahihi la ugonjwa unaoumwa kulingana na dalili ulizonazo.

Kulazimisha Matibabu Fulani. Moja ya kitu kinachowakasirisha madaktari wengi ni kupangiwa aina ya matibabu mfano mgonjwa kulazimisha kuchomwa sindano bila ya kukidhi vigezo na masharti ya sindano, au kung’ang’ani kupwewa aina Fulani ya dawa hasa dawa za kutuliza maumivu na kuleta usingizi.

Ukaidi: Kuna baadhi ya wagonjwa hukataa vipimo, dawa Fulani na baadhi ya matibabu kama upasuaji na kudungwa sindano lakini bado wanataka madaktari wawape matibabu bora. Mgonjwa anapokataa baadhi ya matibabu daktari huchukia na kushindwa kutoa huduma bora.

Kuuliza maswali mengi: Kumuuliza daktari wako maswali mengi na kuwa mashaka na daktari hufanya hatua zote za huduma/matibabu kuharibika. Ni hali ya kawaida kuwa na hamu ya kutaka kujua bainisho la ugonjwa wako na matibabu yake, ingawa si lazima kuuliza maswali kila hatua ya matibabu utkayopitia. Ni vyema kuwa na oradha fupi ya maswali utkayomuuliza daktari na sio kuuliza kila swali.

Kutokuwa na heshima: Kuna baadhi ya wagonjwa huamini madaktari na waaguzi wapo kuhudumia wagonjwa tu hata iweje ndio maana wengine huwa wakali na kutoheshimu wahudumu wa afya na kulazimisha kila wanachotaka.

Kumuomba daktari akutunzie siri kwa watu wako wa karibu. Kuna baadhi ya wagonjwa huwamba wahudumu wa afya kutosema baadhi ya habari za mgonwa kwa wanafamilia au ndugu zake hasa wakiwa wanaumwa magonjwa kama UKIMWI au magonjwa mengine ya zinaa.

Kutohudhuria kliniki kama inavyotakiwa. Ikiwa ni mtoto, mjamzito au mgonjwa ambaaye anapaswa kuhudhulia kliniki kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya mgonjwa, asipohudhuria basi daktari atakasirika sana na kushindwa kutoa huduma bora.

Kuchelewa kutafuta huduma za afya. Watu wengi hufika kwenye vituo vya kutolea huduma wakiwa katika hali mbaya kitu kinachfanya matibabu kuwa magumu kulinganisha na mgonjwa ambaye angefika mapema, hali hii huwakasirisha sana madaktari.

Ni mambo gani ambayo daktari akiyafanya anaweza kumfanya mgonjwa asijisikie vizuri na pengine hata asiamini au asitumie dawa atakazopewa?

Daktari kutomsikiliza mgonjwa kwa makini. Ikiwa mgonjwa ataanza kuongea na daktari, mgonjwa hupenda asikilizwe kwa makini huku daktari akimuangalia mgonjwa uso kwa uso.
Mgonjwa kusubiri kwa muda mrefu bila sababu ya msingi. Wagonjwa wote wanapenda kuhudumiwa haraka zaidi bila kujali idadi ya wagonjwa waliopo, hivyo kama daktari atachelewa kumhudumia mgonjwa lazima mgopnjwa alalamike.
Daktari kutotoa habari kamili kuhusu matibabu ya mgonjwa wake. Wagonjwa wengi wanapenda waelekezwe kwa makini matumizi ya dawa zao kabla hwajaondoka vituo vya kutolea huduma.

Ni maudhi gani ambayo mgonjwa anaweza kuyapata kutoka kwa muuguzi?

Muuguzi kufuatilia na kutoa dawa kwa wakati. Muuguzi asipotoa dawa kama mgonjwa alivyoelekezwa na daktari inaweza kusababisha wagonjwa kuchukia huduma inayotolewa na wauguzi. Muuguzi kutotoa taarifa kamili juu ya matibabu ya mgonjwa. Hii inatia ndani matumizi sahihi ya dawa alizopewa kwa ajili ya afya yake. Wagonjwa wengine wanapenda wahudumu wa afya wawaelekeze kila kitu hasa unywaji wa dawa.

Ni maudhi gani ambayo muuguzi anaweza kuyapata kwa mgonjwa?


Kutotumia vizuri nafasi unapoonana na muuguzi. Ikiwa muuguzi atapita ulipo na kukuuliza kama utahitaji msaada wake ni vyema kusema shida yako wakati huo na sio kusubiri wakati ambapo ameondoka ndio umuite. Kulalamika pale unapomuona daktari. Muuguzi huchukia wagonjwa wanaosema malalamiko ya ugonjwa wao kwa madaktari punde tu wnapowaona madaktari wakati muda wote walikuwa na waaguzi hawakusema matatizo yao au jinsi wanavyojihisi.


Familia au ndugu kuingilia matibabu ya mgonjwa. Ikiwa mgonjwa atalazwa wodini ili kuendelea na matibabu, wauguzi hawapendi kuingiliwa na familia ya mgonjwa katika utoaji wa huduma zao mpaka watakapohitaji msaada wa familia.

 
Top