afya ya viungo vya uzazi

 Una Tatizo Kuhusu Sehemu Nyeti?
 Mada ya leo ni ya utangulizi kuhusu mambo mbalimbali tutakayoyajadili katika sehemu hii ya tovuti yetu. Sehemu hii  ni mahsusi kwa ajili ya mambo yanayohusiana na afya ya sehemu nyeti za mwanamme na mwanamke. Hili linatugusa tulio wengi au kila mmoja wetu kwa namna moja au nyingine. Kuna masuala mengi sana hapa yakuyajadili na najua itanichukua muda mrefu sana kukamilisha na kugusia yote. Nitaanza taratibu na kila siku kuongeza kitu fulani hadi hapo tutakapofikia kiwango kizuri. Siwezi kuwa na vipengele vyote mimi binafsi, hivyo naomba wewe kama msomaji utoe maoni au kuuliza swali ili niongeze kile ambacho sijakiweka hapa. Kwa kuanzia, hapa chini ni orodha ya vipengele vya kuanzia na kila kimoja tutakijadli kipekee katika kurasa za huko mbele.

 Afya Ya Sehemu Nyeti Za Mwanamme

Matatizo yanayotusumbua sisi Wanaume yammeorodheshwa hapa chini. Kama kuna tatizo ambalo linakusumbua na halijaorodheshwa hapa chini, tafadhali usisite kuniandikia. Nitakujibu, nitaliorodhesha na kulifanyia kazi. Ushirikiano wako msomaji wa tovuti hii, ndio kuiboresha tovuti yetu.

 Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa (Loss Of Libido)

Hapa titajadili sababu ambazo zinapelekea baadhi yetu kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa (kwa lugha ya mtaani, kukusa nyege) na kisha kuona ni nini unaweza kufanya au vitu gani unaweza kuvitumia ili kuibadlili hali hiyo. Katika ukurasa mmoja tutaonasababu za mwanamme kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa na katika ukurasa mwingine tofauti tutajadili sababu za mwanamke kukosa hamu ya kufanya mapenzi.

Kukosa nyege

 Jogoo Kushindwa Kuwika

Tatizo la jogoo kushindwa kuwika au jongoo kushindwa kupanda mtungi ni hali ambayo mwanamme anakuwa nayo ambapo  mtu huyu anapenda kufanya tendo la ndoa lakini sehemu nyeti zinamwangusha au kwa kukataa kabisa kuwa tayari kwa tendo hilo au mara nyingine kuwa tayari lakini kwa muda mfupi sana. Kwa baadhi ya watu, sehemu zao hukosa kufika wima kabisa (full erection).

jogoo kushindwa kuwika

 Kufika Kileleni Mapema (Premature Ejaculation)

Tatizo la kuwahi kufika kileleni ni tatizo ambalo mtu akiwa nalo huanza tendo la ndoa na mara ghafla alishamaliza. Ulishamwona jogoo? Kwa binadamu hili ni tatizo. Kuna tiba ambayo mtu akitumia, tatizo hili huondoka. Pia mwanamme anaweza kufanya mazoezi ya Kegel kuondoa tatizo hili.

kuwahi kufika kileleni

 Kuwa Na Kiwango Kidogo Cha Mbegu (Low Sperm Count)

Mbegu za mwanamme (manii) huwa zinatakiwa ziwe na ujazo fulani. Mwanamme ambaye hatoi manii kufikia ujazo huo, huweza kushindwa kumzalisha mwanamke. Ni nini chanzo na ufumbuzi wake ni nini? Haya yote tutayajadili katika ukurasa tofauti.

mbegu chache

Kuwa Na Uume Mdogo

Mada hii inasumbua wanaume wengi sana –  dunia nzima. Jee, kuna madhara yo yote ya kuwa na maungo madogo? Njia nyingi wanaume wamejaribu kuzitumia ili kuongeza urefu na upana wa sehemu zao za siri. Njia hizo ni pamoja na mazoezi (Jelq Technique), Vacuum Pumps, Extenders, Vidonge, creams n.k. Njia zipi ni bora? Hayo yote yanachambuliwa kwa kina ndani ya ukurasa wake.

 Afya Ya Sehemu Nyeti Za Mwanamke


 Miwasho Ya Sehemu Nyeti Za Mwanamke

Miwasho ya sehemu nyeti za mwanamke inatokana na sababu nyingi na tiba yake itategemea tatizo litakaloonekana. Dawa mbalimbali zimetengenezwa kukumbana na tatizo hili.

sehemu nyeti za mwanamke

 Kutoa Uchafu Na Kutoa Harufu Sehemu Nyeti Za Mwanamke

Wapo wanawake wengi sana wanaosumbuliwa na tatizo hili. Ni tatizo linaloweza kusababisha mwanamke kutorokwa na mwenzi wake, lakini bahati nzuri ni tatizolinalotibika.

 Kuwa na Uchi Mpana (Uchi Kulegea)

Hili ni tatizo ambalo mara nyingi sana hutokana na uzazi. Mwanamke akipatwa na tatizo hili huweza kukimbiwa na mwenzi wake. Kuna baadhi ya dawa zimetumiwa sehemu mbalimbali ulimwenguni kupunguza au kuondoa tatizo la kuwa na uchi mpana au uchi kulegea. Zipo dawa za kutumia kabla ya tendo la ndoa na zingine ni za kutumiwa kama dawa nyingine za kawaida. Yapo piamazoezi ya kufanya ili kuimarisha misuli ya sehemu nyeti ili kuondoa tatizo hili. Una tatizo hili? Wasiliana nasi tukupe ushauri.
Usisite kutoa maoni, ushauri au kuuliza swali kuhusiana na mada hii. Hii ni tovuti yako Mtanzania, mchango wako ndio utakaoiboresha tovuti yetu.

 
Top