Faida za matumizi ya vipodozi asilia
Vipodozi asilia vimekuwa vikishindana kwa kasi na vile vya kemikali. Kwa kutengenezwa kwake na viungo asilia, vipodozi hivi vimekuwa vya uhakika hasa katika kauifanya ngozi yako iwe na afya njema na mwonekano mzuri wa kuvutia.
Pamoja na sifa hizo, vipodozi hivi ni rafiki wa mazingira. Hivyo unaweza ukaagana na matumizi ya kemikali zinazosababisha madhara mabalimbali katika ngozi yako.
Zipo faida mbalimbali zinazopatikana kwa utumiaji wa vipodozi asilia. Baadhi yake ni :
Havina athari
Kwa kuwa vipodozi hivi hutokana na mimea asilia, ngozi yako itaweza kupata tiba bora asilia ambayo husaidia kupambana na maradhi na kuboresha mwonekano wa ngozi yako.
Kuifanya ngozi iwe na afya
Vipodozi asilia hufyonzwa kwa urahisi katika ngozi yako, hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kufungua matundu ya hewa na kuifanya ngozi yako kupumua kwa nafasi.
Kutungeneza ngozi
Vipodozi hivi pia vina sifa ya kukarabati ngozi hasa ile iliyoathirika. Inawezekana kutokana na matumizi ya vipodozi vyenye kemikali hatari au hata kutotumia vipodozi kwa usahihi ngozi yao ikaathirika, lakini vipodozi vya asili hutengeneza ngozi yako, hata kuirejeshea uasili wake.
Ukadiriaji wa muda wa matumizi
Tofauti na vipodozi vyenye kemikali, vipodozi asilia hutengenezwa kukidhi mahitaji ya mtumiaji. Unaweza kutumia vipimo kulingana na mahitaji yako. Pia ni juu yako kukadiria muda wa matumizi.
Rafiki wa mazingira
Wataalamu wa urembo wa asili wanashauri matumizi ya vipodozi asilia kwani ni rafiki wa mazingira.
Dondoo za utengenezaji wa vipodozi asilia Mask au srub : Tumia mchanganyiko wa asali, mtindi na oatmeal kwa kiwango sawa. Ni scrub bora zaidi kwa ajili ya ngozi za aina zote. Pia unaweza kutumia asali kwa kualainisha ngozi yako ya uso.
 
Top