Somo hili nimeliandaa hasa kwa madhumuni yafuatayo:
*Kutoa elimu kwa mwandaaji wa chakula cha familia kuwa chakula anacho andaa basi kiwe hakija poteza uhalisia kuwa tiba mwilini.
*Kufundisha jamii namna gani CHAKULA ASILI kinaweza kutumika kama tiba na kukuepusha na magonjwa mbali mbali.
*Kukufundisha namna gani unaweza kuandaa chakula chako asili ambacho kitakusaidia kuondoa athari ya vyakula mbali mbali zinazopelekea kupata magonjwa mbali mbali kama uzito kupita kiasi, kisukari,shinikizo la damu, vichocheo vya kike kuvurugika nk
*Tutakupatia faida mbali mbali ya vyakula katika mlo wako wa kila siku.
Hivyo basi uandaaji wa chakula ambacho ni bora kwa afya yako inahitaji elimu sahihi ili kuweza,kuwezesha mwili wako kurudisha na kuimarisha utendaji kazi wake.
Kitu ambacho nataka nikwambie ni kuwa mfumo wa CHAKULA ni mfumo unaounganisha mifumo mingine yote. Nina maana kuwa endapo mfumo huu ukiathiriwa mifumo yote mingine ya mwili inavurugika ndio maana sasa sisi kama wataalamu wa vyakula na waandaji wa kipindi hiki tumeona ni jukumu letu kukupa msaada huu kuhakikisha tunaimarisha mfumo wako wa chakula katika utendaji kazi wako.
Basi leo tujifunze NAMNA YA KUANDAA JUICE YAKO SAFI KABISA NYUMBANI KWAKO YENYE FAIDA KIAFYA:
KWA NINI TUNAHITAJI JUISI?
*Unywaji wa juisi ya matunda na mboga mboga unatusaidia kupunguza kiwango cha mboga mboga na matunda na kuyaweka katika glasi tu. Hivyo badala ya kula mboga beseni zima unaweza kukamua ukapata glas mbili ukanywa kama juisi.
*Kwa kawaida unashauriwa upate matunda na mboga mboga zaidi ya aina tatu kwa kila mlo. Sasa kutokana na uchumi hatuwezi kuhakikisha hili unatekeleza na hivyo tunakuwa tuna ishi na miili yetu iliyopungukiwa vitamini na madini mbali mbali mwilini mwetu. Upungufu wa madini muhimu mwilini km manganese, chuma na vitamini muhimu zinafanya mwili kutotekeleza shughuli za mwili ipasavyo. Hivyo vitu navifananisha km mbolea za mwili zinazofanya shughuli zote za mwili zienda ktk usawa unaotakiwa. Kupungukiwa kwa matunda na mboga mboga kunasababisha mwili kushindwa kuunguza mafuta mwilini vizuri, kushindwa kuondoa takamwili na magonjwa mbali mbali ya kimwili.
kupitia unywaji wa juice UNAJIPATIA VITAMIN NA MADINI MENGI hii pia ni nzuri zaidi kwa wale wavivu wasiopenda kula mboga na matunda kupitia juice wataboresha miili yao na kupata madini yote na vitamini zote
* Juisi za matunda na mboga mboga zina sifa hizi kubwa kabisa,
~Hazina kabisa cholesteral(ziro cholesteral)
~Hazina mafuta
~Hazina sukari nyingi
~Zina madini mengi na vitamini nyingi.
~Zinaondoa athari zote za vyakula vya viwandani na kurudisha uwezo wa mwili wako ku unguza mafuta mabaya yote na shuguli zote kufanyika ipasavyo.
NAMNA YA KUANDAA JUISI YAKO KWA MLO WAKO WA NYUMBANI:
Baada sasa ya kujifunza kwa nini tunahitaji juisi miilini mwetu basi tujifunze namna ya kutayarisha na kuandaa matunda na mboga mboga ili uweze KUTENGENEZA JUISI NZURI KWA MATUMIZI YAKO YA NYUMBANI
MAHITAJI
~MBOGA ZA MAJANI
Mfano: Kabeji,spinach nk
~Matunda
Mfano: Ndizi, apple, chungwa nk
~Vionjo asili
mfano:Mdalasini, tangawizi , kitunguu swaumu. Nk
~Maji ya kuoshea
~Kisu
~Kikamua juisi (Juicer)
*Kama hizi ni mboga mboga au matunda umelima kwa kutumia mbolea na dawa za viua wadudu asili nakushauru unaosha vizuri kisha unapunguza ukubwa wa bonga zako au matunda kwa kutumia kisu chako na hakikisha vipande hivyo vinaweza kuingia vizuri kwenye blender yako
*Kama huna uhakika na matunda hayo ulimwaji wake na hizo mboga mboga .mfano kabeji unaweza kuondoa kwanza yale maganda ya juu ili kuepusha kukamua juisi yenye viambata vya viua wadudu(chemical pesticides). Hivyo itakusaidia baada ya kuondoa maganda ya juu au layer ya juu basi osha kwa maji mengi sana kuondoa hizo kemikali za dawa.
AINA YA VIFAA VYA KUKAMULIA JUISI
Watu wengi tumekuwa tukiitumia juisi kama vinywaji vingine tunavyotumia kwenye sehemu za starehe.
Hivyo basi LEO TUTAJIFUNZA MAAJABU YA JUICE ILIYOTENGEZWA KUFUATA MASHARTI NA UKABORESHA AFYA YAKO UNAPOKUWA UNAPATA MLO WAKO WA KILA SIKU.
Vifaa vya kutengenezea juisi vipo vya aina mbali mbali lakini katika makala hii nitasema kwa ufupi kuhusu vifaa hivi vya kutengenezea juisi zetu ili tuone kama ni salama kwa matumizi yetu:
1. CENTRI FUGAL JUICER
Hii ni aina ya kikamua juisi ambacho ndani kuna kifaa kinachozunguka kwa kasi na kutoa sauti kwa nguvu. Aina hii ya kikamua juisi hutumika kusaga juisi yako yote na pia ni kifaa ambacho hakipotezi uhalisia wa nyuzi nyuzi za matunda yako.
Nyuzi nyuzi hizo hufanya tumbo la chakula kushinda kwa muda mrefu likiwa limejaa na hivyo kutolewa kwa kichocheo cha leptin na seli zakuhifadhi mafuta ambayo inaenda kwenye ubongo na kukata hamu ya chakula na hatimaye kuzuia ulaji wa mara kwa mara ambao huchangia uchovyaji wa insulin kwa wingi na kusababisha mafuta mengi kuhifadhiwa pamoja na kuvurugika kwa vichocheo.
Hivyo ulaji wa matunda na mboga mboga zenye nyuzinyuzi (fiber) kwa wingi ni muhimu sana kuondoa tatizo kwa wanao shinda wanakula mara kwa mara na wale wanao taka kupunguza uzito.
**Hasara Za Kikamua Juisi Cha Centri Fugal**
Kile kibati kinazunguka kwa kasi sana hivyo huchemka na hatimaye kuongeza joto na hewa ya oksijeni ambayo inaweza athiri viini (Nutrients) mahususi vya juisi yako. Hivyo ili uweze kupata viini vyako unapokuwa unatumia kikamua juisi hiki hakikisha kuwa unakunywa juisi yako mara tu baada ya kuitengeneza au unaweza kuhifadhi kwenye kibebeo ambacho kina mfuniko imara sehemu yenye giza au mwanga hafifi kwani juisi huathiriwa na mwanga na hewa.
Ukikiuka utaratibu huo ni dhahiri kuwa juisi itakuwa haitumiki kama tiba kiafya bali itakuwa kama kinywaji cha kwenye majumba ya starehe.
Kikamua Juisi hiki kinapokuwa kinazunguka kwa kasi kinapiga kelel sana hivyo inaleta usumbufu kwani hakuna sehemu ya kupunguzia kelele.
Kumbuka kuwa vikamua juisi vya aina hii ndivyo vitumikavyo mara kwa mara kwani vinauzwa kwa bei ya chini kidogo na kila mtanzania anaweza kumiriki. Hivyo kama na wewe unatumia aina hii ya kikamua juisi fuata masharti mazuri kabisa.
2. COLD PRESS JUICER
Hii ni aina ya kikamua juisi ambayo ina mfumo wa hali ya juu wa kukamua juisi pia hutenga nyuzi nyuzi na kubakiza na juisi peke yake.
Pia aina hii ina uwezo mkubwa wa kutoa viini vyote vya lishe yani Nutrients na pia utumiapo mashine hii utajipatia kiwango kingi cha juisi kuliko ungetumia CENTRIFUGAL.
Kikamua juisi hiki hakipigi kelele kabisa na una uwezo wa kuihifadhi juisi iliyo tengenezwa mashine hii kwa muda wa masaa 72 bila kuathiri viini vya lishe; kwani haizalishi joto kama aina nyingine hivyo hulinda sana viini vya tunda na mboga mboga.
Pia aina hii ya kikamua juisi ni nzuri sana kwa wale wanopenda kutumia kupata juisi ya mboga za majani kama spinach, kabeji kwani ina uwezo wa kusaga vizuri na kukupatia juisi iliyo sheheni viini vya lishe.
INA UWEZO WA KUKAMUA JUISI ZAIDI YA ASILIMIA 20-25 UKILINGANISHA NA AINA YA KWANZA
**™Hasara Za Kikamua Juisi Hiki**™
Inaondoa nyuzi nyuzi kwenye juisi yako na hivyo basi utumiapo juisi hii tambua kuwa ni juisi ambayo ina nyuzi nyuzi kidogo sana na hivyo inaweza kukufanya sukari yako iwe imepanda muda wote na kukufanya uzito wako kuongezeka,kuchoka na mengine mengi.HIVYO SIO NZURI SANA KIAFYA
Ni gharama sana kuinunua kwani mtu mwenye kipato kidogo hawezi kumudu kuwa nayo.
Zingatia:
Tafiti zinasema kuwa juisi nzuri ni ile inayohifadhiwa katika chupa ya kioo na sio chupa au galoni ya plastic. Hivyo ningependa wewe unaye taka kuhifadhi juisi yako fuata masharti hayo ili uweze fikia malengo yako kiafya.