JINSI YA KUEPUKANA NA CHUNUSI KWA HARAKA ZAIDI
Chunusi zimekuwa ni hali ya kawaida katika ngozi ambazo watu wengi sasa huathirika na hizo. Hali hii ya kuharibika kwa ngozi hutokea pale matezi ya Sebaceous (oil glands) yaliyokuwa katika ngozi huathiriwa na vijidudu, kuvimba na kutunga usaha. Huonekana sana sehemu za usoni, shingoni, mgongoni na hata kwenye mabega. Ingawa sio hali ya hatari kwa wanadamu lakini chunusi huwafanya watu kuonekana wabaya kutokana na muonekano wake.
Katika maduka kuna losheni na madawa mengi san akwaajili ya kutibu chunusi, lakini inaweza kuchukua muda sana na hata baadaye ukashindwa kugundua ni dawa ipi iliyokutibu kutokana na kutumia dawa hii na ile.
Hata hivyo kuna njia 7 za kiasili ambazo zinaweza kukusaidia katika kuondoa chunusi hizi kwa haraka sana.
Njia ya 1. kutumia barafu.
Chukua kipande cha barafu au vipande vidogo vidogo, kasha vifunge katika kipande cha kitambaa kasha kanda uso wako kwa upole kabisa sehemu zilizoathirika na chunusi kwa muda wa sekunde kadhaa hivi. Hii itasaidia katika kuondoa uvimbe uvimbe katika sehemu hizo.
Njia ya 2. kutumia limao,
Ile Vitamin C iliyopo katika limao husaidia sana katika kuondoa chunusi kwa haraka, unachotakiwa ni kutumia maji ya limao yaliyo fresh (usiyalaze maji hayo kwa matumizi ya baadaye) kasha upake sehemu zilizoathirika kila ukitaka kulala usiku. Hii itasaidia katika kukausha ngozi yako kutokana na mafuta yanayosababisha uvimbe. Asubuhi unachotakiwa ni kwenda kunawa na maji ya vuguvugu. Hata hivyo njia hii siyo nzuri kwa wale wenye ngozi laini sana.
Njia ya 3. kutumia asali,
Paka asali sehemu zilizoathirika kwa kutumia kitambaa safi na laini, kasha kaa kwa muda wa dakika thelathini (nusu saa) baada ya hapo osha sehemu hiyo kwa utaratibu kabisa kwa maji safi. Pia uukipata unga wa mdalasini, changanya na asali kasha pakaa unga huo uliochanganyika na asali katika sehemu iliyoathirika kila unapotaka kulala usiku, asubuhi utaona matokeo mazuri, kisha osha na maji ya baridi.
Njia ya 4. kutumia dawa ya meno (Toothpaste),
Hii dawa ya meno unayoitumia kila siku kupigia mswaki inaweza kusaidia sana katika kuondoa chunusi haraka. Kwa matibabu ni lazima utumia dawa nyeupe na epukana na zenye gel, pakaa dawa hii katika sehemu iliyoathirika kila unapotaka kwenda kulala na kisha osha vizuri uso wako asubuhi, utagundua maendeleo mazuri katika sehemu hiyo iliyoathirika, kama unaweza pia kutumia mchana basi hakuna ubaya wowote lakini njia hii inatakiwa itumike baada ya kutumia njia ile ya barafu. Na pia lazima uhakikishe kwamba dawa hii inakaa kwa muda wa nusu saa baada ya kuipaka ndiyo unawe.
Njia ya 5. kutumia mvuke,
Njia hii husaidia sana kuzibua vitundu vidogo vidogo vilivyoziba kwa uchafu na kuruhusu hewa nzuri kuingia katika ngozi. Hii husaidia ngozi kuepukana na mafuta, uchafu na vijidudu ambavyo hukaa sana katika vitundu vya ngozi na kusababisha madhara kama haya ya kuvimba na kuleta chunusi. Chukua beseni na liwekee maji ya moto yenye kutoa mvuke na jifukize ukiruhusu mvuke kuingia katika sehemu zilizoathirika kwa dakika chache, mwisha osha uso wako kwa maji ya kawaida na baada ya kukausha, paka mafuta ya kulainisha ngozi (moisturizer). Njia hii itakusaidia pia kuonekana mng’aavu katika uso wako.
Njia ya 6. kutumia kitunguu saumu,
Hiki husaidia katika mambo mengi sana ya matibabu katika mwili wa binadamu kwani kitunguu saumu kina faida nyingi sana. Hiki kina sulphur ambayo ina faida sana katika kutibu chunusi. Chukua kidole cha kitunguu saumu na kikate katika vipande viwili kisha kipake katika sehemu zilizoathirika kwa muda wa dakika tano kabla ya kuosha kwa maji ya vuguvugu. Mchakato huu ukitumika mara kwa mara husaidia kuondoa chunusi kwa haraka sana na bila kuacha athari zozote zile katika ngozi. Na pia ukila kidole kimoja cha kitunguu saumu kila siku ina manufaa makubwa sana kama vile kusafisha damu, lakini usile sana kwani unaweza kuchafua tumbo.
Njia ya 7. kutumia Baking Soda,
Hii pia ni njia ya haraka ya kuondoa chunusi, hii Baking Soda haina kemikali mbaya hivyo haitaleta madhara yoyote katika ngozi yako hata kama una ngozi laini sana. Weka kiasi cha kijiko kimoja cha chai unga huu wa Baking Soda na changanya na maji kidogo au maji ya limao hakikisha usiwe mlaini sana yaani unatakiwa uwe uji mzito. Kabla ya kuweka hakikisha umeosha ngozi yako vizuri kabisa kuondoa uchafu ndani yake, kisha paka mchanganyo huo katika sehemu iliyoathirika na acha mpaka ikauke kwa dakika chache. Usiache ikae kwa muda mrefu katika ngozi kwani inaweza kusababisha ukavu katika ngozi. Kisha osha vizuri kwa maji ya uvuguvugu na paka mafuta ya kulainisha ngozi (moisturizer). Rudia mchakato huu mara mbili kwa siku kwa matokeo ya haraka.
Njia ya 8. kutumia Tango,
Hili lina vitamin A, C, E na Potassium ambayo husaidia katika kutibu chunusi, vile vile kulipaka katika ngozi pia husaidia sana. Chukua tango jipya moja au mawili, kata vipande vipande na loweka katika maji safi ya kiasi kwa muda wa saa nzima, vile virutubisho vinavyopatikana katika tango vitahama katika maji. Chuja maji yale na uyanywe. Vilevile unaweza kutumia maji haya kwa kuoshea uso wako. Pia unaweza kuchukua tango na kulisaga kisha ukapaka katika uso wako na kuacha kwa dakika kadhaa kisha ukaosha kwa maji safi ya vuguvugu. Njia hii itasaidia kusafisha vitundu vya ngozi na kuondoa vijidudu vilivyo katika matezi ya mafuta yaliyo ndani ya ngozi.
Kwa upande wangu ni hayo tu, ikiwa una lolote la kuongezea si vibaya ukachangia ujuzi wako hapa, kwa maswali, maoni na ushauri jisikie huru kutuandikia. Unaweza kujiunga nasi na ufaidike na mengi kutoka kwetu na ukutane na kujadiliana na watu mbalimbali kuhusu mada tofauti katika ukurasa wetu wa Forum, jisikie huru kujiandisha sasa. Ahsante