SOCIAL HALL
Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaowapata wanawake wajawazito, hasa wenye mimba za kwanza. Kwa walio wengi, ugonjwa huu hutokana na kupanda kwa msukumo wa damu (High blood pressure). Ugonjwa huu utokeapo, mgonjwa hupatwa na degedege (convulsions). 

Kifafa cha uzazi au wengine wanakiita kifafa cha mimba ni miongoni mwa matatizo
yanayosababisha vifo vya wajawazito nchini.Kifafa cha mimba kinaweza kutokea wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au baada
ya kujifungua.
SABABU ZINAZO PELEKEA TATIZO HILO.

Sababu la tatizo bado wataalamu wa tiba duniani hawajagundua. Ila kuna baadhi sababu zinahisiwa kusababisha tatizo hili
(Predisposi ng factors). Baadhi ni pamoja na


1.Mwanamke kuwa na wenza wengi hali inayopelekea muingiliano wa Chromosomes.
2.Sehemu moja ya ubongo kuwa na damu nyingi kuliko nyingine na kupelekea shinikizo la damu kuwa kubwa katika ubongo.
3 Mimba ya kwanza, hususan katika umri mdogo chini ya miaka 20 na umri mkubwa zaidi ya miaka 35. 
4 Wenye mimba ya mapacha hupata zaidi kuliko mimba ya mtoto mmoja. 
5 Ugonjwa wa shinikizo la damu au kisukari kabla ya kubeba mimba. 
6 Kuwa na ugonjwa wa figo kwa mama mjamzito.

SABABU NYINGINE PIA NI KAMA

 1.wanawake wote wenye mimba za kwanza 
2.mimba za mapema kabla ya 20
3. wanawake ambao wazaz,bib au ndg zao wa karbu waliwah kupatwa na matatzo ya kifafa katka mimba zao
4. wanawake walev hasa wakiwa wajawazito
5.wavutaj wa sigara
6. wanawake wenye visukar
7.wanawake wenye presha
8.mimba za uzeeni baada ya miaka 35
9.wanawake wenye tabia ya kubadlisha badlisha wanaume
10.wanawake waliopatwa na kfafa mimba zao za kwanza kuna hatar kukpata kifafa tena mimba znazofuata
11.mimba za mapacha
12.kuzaa mara nyingi 
DALILI ZA KIFAFA CHA MIMBA

1.Kuvimba na kubonyea kwa miguu(Pitting Oedema).

2.Shinikizo la damu kupanda.

3.Kuwa na protein katika mkojo.

4.Kizunguzungu na macho kuoana giza.

5.Kifafa chenyewe cha mimba.

MADHARA YA KIFAFA CHA MIMBA.

1.Mama mjamzito anaweza kupoteza maisha yeye na mtoto wake.

2.Kuzaa mtoto mfu.

3.Mama kuendelea kuwa na tatizo la kifafa maisha yako yote. (Epilepsy)

4.Mama kuendelea kuwa na tatizo la shinikizo la damu la kupanda.(High blood pressure)

5.Kuzaa mtoto mwenye uzito 
pungufu.

SULUHISHO

 1.Kujifungulia katika kituo cha afya.

2.Kuhudhuria Klinik wakati wa ujauzito.

3.Kumuona daktari unapokuwa na viashiria vya hatari wakati wa ujauzito kama kuvimba miguu au shinikizo la damu kupanda
 
Top