1. Osha uso wako kila siku na sabuni ta kusafishia uso ambayo haina chemicals na kamwe usitumie sabuni ambayo itaondoa uhasilia wa mafuta kwenye ngozi yako.
2. Kila siku tumia vilainishaji ngozi wakati wa mchana na unapopaka kilainishi kwenye ngozi yako massage ngozi yako kwa mduara kwa kwenda juu na sio kuvuta au kusugua ngozi yako.
3. Unatakiwa kupaka cream kwenye ngozi yako kabla ya kwenda kulala maana ni vyema kutumia cream ambazo zina Alpha Hydroxy Acids au AHA`s ambazo zinajulikana ambazo zinatokana na vyanzo kama vile maziwa, matunda na sukari. Hizi Alpha Hydroxy Acids zinakausha, zinaua na zinaondoa tabaka la ngozi ya nje wakati zina zinalainisha ngozi mpya inayotoka.
Faida yake ni kwamba ngozi yako inaonekana kuwa nzuri na ngavu pia ngozi yako kung`aa na kuwa na rangi nzuri. Kwa pamoja AHA na Vitamin C husaidi kupunguza mishati na ishara nyingine ya aging hivyo unaweza kupata matokeo mazuri na kwa haraka kwa kutumia vilainishi au cream ambavyo vina Vitamin C wakati wa mchana na cream ambazo zina AHA wakati wa usiku.Kwa kawaida tumia bidhaa ambazo zinakua zenye moisturiser na cream.
4. Kama ngozi yako ni kavu na inaelekea kuwa na mistari na inaonekana nyekundu na inakua inauma au ina vipele unatakiwa kumuona daktari wa ngozi. Hali hii pia inaweza kusababishwa na hali ya hewa au kusababishwa na vitambaa kama vile pamba, vitu tunavyopaka kwa ajili ya kutunza ngozi au sabuni na kadhalika.
Daktari anaweza kukushauri ni cream gani utumie kulainisha ngozi yako na kuondoa wekundu kwenye ngozi yako pia kuondoa bugudha kwenye ngozi yako kama vile kutumia vitambaa vya cotton na kuepuka Watu wengi wanapata matatizo kuwa na ya ngozi kavu hasa kutokana na hali ya hewa. Kama ni miezi ya baridi husababisha ngozi yako kuwa kavu hivyo matumizi ya mara kwa mara ya vilainishi vitasaidia ngozi yako kuwa ngavu na nyororo.