Hypertension ni nini? Huu ni ugonjwa ambao hugunduliwa pale presha ya damu inapokua juu sana kupita kiwango chake cha kawaida.

Kawaida damu inasukumwa na moyo kwenda sehemu mbalimbali za mwili lakini nguvu inayotumika kusukuma damu hiyo  kutoka moyoni kwenda sehemu zote za mwili na ile ambayo inakuwepo kwenye mishipa ya damu wakati damu inapita ndio inaitwa presha ya damu. Hivyo binadamu yeyote lazima awe na presha ya damu lakini katika kiwango kinachohitajika ambacho ni 120\80mmhg mpaka 140\90mmhg zaidi ya hapo tunaita hypertension..

WALIOKO KWENYE HATARI YA KUPATA PRESHA..
umri mkubwa: wanaume wako katika hatari ya kupata presha kwenye umri wa miaka 45 na kuendelea na wanawake miaka 65 na kuendelea.

Rangi ya ngozi: presha ya damu inasumbua sana watu weusi na huweza kuanza katika umri mdogo zaidi na madhara makubwa kama kupooza, moyo kusimama ghafla na kufa kwa figo hutokea kwa weusi kuliko weupe.

Familia; Koo zenye wagonjwa wengi kwa presha kwani ugonjwa huu hufuata koo wakati mwingine

Unene: kadri unavyozidi kunenepa ndivyo mwili moyo unataka nguvu nyingi kusukuma damu
mwilini hivyo kuongezeka kwa presha.

Kutofanya mazoezi
Kuvuta sigara: kemikali ya nikotini huharbu mishipa ya damu na kuongeza hatari ya kuugua ugonjwa wa presha.

Kula chumvi nyingi; sodium hubakiza maji mengi mwilini na kuongeza presha ya damu.

Kunywa pombe sana; kunywa zaidi ya bia mbili kwa wanaume na zaidi ya bia moja kwa wanawake ni hatari kwa moyo na hupandisha presha ya damu.

Mawazo mengi; mawazo mengi humwaga homoni inaitwa adrenaline kwenye damu ambayo huongeza presha ya damu hivyo maisha usiyachukulie serious sana matatizo ni sehemu ya maisha.

Magonjwa Fulani Fulani: magonjwa kama kisukari na magonjwa ya figo huongeza hatari ya kuugua presha ya damu.


Kuna aina mbili za presha ya kupanda..

  1. Primary hypertension: ambayo inakumba zaidi ya 95% ya watu na chanzo chake hakifahamiki.
  2. Secondary hypertension: ambayo inakuwepo kwa 5% ya watu na chanzo chake kinafahamika na ambavyo ni magonjwa ya figo, magonjwa ya mishipa ya damu, magonjwa ya ubongo na mishipa ya fahamu na magonjwa ya mfumo wa homoni.


dalili zake ni zipi?
Dalili za presha mara nyingi hua hazipatikani kirahisi na ugonjwa huu hauna dalili maalumu na wakati mwingine huja kulingana na chanzo cha presha hiyo kama nilivyoeleza kwenye secondary hypertension kama ifuatavyo.

  1. Kichwa kuuma
  2. Kutokwa damu puani.
  3. Kupumua kwa shida.
  4. Kuishiwa nguvu
  5. Moyo kukimbia sana
  6. Kutokwa jasho kwa wingi


Vipimo vinavyofanyika hospitali..
Kupima presha kwa kutumia kipimo cha presha kitaalamu kama sphygmomanometer ambacho ikiwa mgonjwa atapimwa mara tatu kwa siku tatu tofauti masaa na kukutwa presha yake iko juu ya kawaida atahesabiwa kama mgonjwa wa presha na matibabu yake yataanza haraka. hata hivyo mgonjwa anatakiwa apimwe baada ya dakika tano za kupumzika kama alikua kwenye mizunguko yake.

Vipimo vingine huchukuliwa na daktari kujaribu kujua chanzo cha ugonjwa na madhara ambayo mgonjwa anaweza kua ameshayapata kutokana na ugonjwa huo ni X ray ya moyo kuangalia ukubwa wa moyo, kuangalia wingi wa lehemu kwenye damu{cholesterol}, ultrasound za figo zote kuangalia kama kuna shida yeyote huku, kipimo cha maabara cha mkojo kuangalia kama figo zimenza kupitisha vitu visivyotakiwa kutoka kama damu na kadhalika na kupima sukari kuangalia kama mgonjwa ana kisukari kwani magonjwa haya huambatana mara nyingi..

Matibabu ya presha
Kuna aina kuu za matibabu..

Matibabu yasiyotumia dawa {non pharmacological treatment]
matibabu ya dawa [pharmacological treatment]

hebu tuanze na matibabu yasiyotumia dawa…
punguza uzito: mpaka uzito uwe sawa na urefu wako, naomba nikwambie kama wewe una presha afu ni mnene unapoteza muda kwani ugonjwa huu utakutesa sana na utalazwa mara kwa mara.

Punguza unywaji wa pombe: kunywa pombe kupita kiasi huathiri mifumo mingi ya mwili na kama una presha haitashuka bali itakutesa mpaka ikuue hivyo kama we unakunywa pombe fuata viwango vya kiafya vya kunywa pombe. Bia mbili kwa mwanaume ndani masaa 24 na bia moja kwa mwanamke ndani ya masaa 24 na kila bia moja ikinywewa kwa muda wa saa moja.

Fanya mazoezi angalau nusu saa kwa siku: hii itakusaidia kupunguza mafuta yaliyoganda nadani ya mishipa ya damu na kushusha cholesterol nyingi ambayo ni hatari kwa afya yako. Mafuta haya ndio yanafanya presha ya damu inakua juu na husababisha vifo vya ghafla kwa sababu ya kuziba mishipa inayopeleka damu kwenye moyo.{coronary arteries}

Acha kufuta sigara: sigara inaweka kemikali nyingi za nicotini kwenye mishipa ya dmu amabayo huongeza presha maradufu na hakuna kiwango cha afadhali cha kuvuta kwani kila sigara unayofuta inakupunguzia siku za kuishi.

Acha kula nyama nyekundu zote na mafuta ya wanyama; nyama hizi zina lehemu nyingi au cholesterol, huongeza unene na mafuta mengi mwilini ni hatari sio kwa wagonjwa wa presha tu hata kwa watu ambao hawaumwi presha hivyo kama unataka nyama kula nyama nyeupe yaani samaki wa aina zote na nyama ya ndege wa aina zote mfano kuku[ wa kienyeji ni bora zaidi}, bata, njiwa, kanga, mbuni na kadhalika. Wanyama wote wanaotembea kwa miguu minne usiguse nyama zao. pia tumia mafuta ya mimea kama alizeti, mawese na korie kwani mafuta ya wanyama kama siagi ni hatari kwa afya yako.

Acha au punguza ulaji wa chumvi kwa kiasi kikubwa sana: hichi ndio kitu kikubwa ambacho wengi hawakijui, kama unaumwa presha hakikisha unakula mboga zako tofauti na watu wengine zikiwa hazina chumvi kabisa au chumvi kidogo mno, chumvi ina kimelea kinaitwa sodium ambacho huvuta maji ndani ya mwili na kupandisha sana prresha hivyo kama wewe ni mgonjwa wa presha na unatumia chumvi ujue unapoteza muda. Kuna chumvi maalumu kwa ajili ya wagonjwa wa presha ambazo zina sodium kidogo ana hizo unaweza kula unavyotaka.Chumvi hizi zinapatikana mijini mikubwa Tanzania hivyo kama wewe ni mgonjwa wa presha na uko mikoani tunaweza kukuagizia popote ulipo kama ukihitaji.

Matibabu ya dawa{ pharmacological treatment}
Mgonjwa atakapobainika na ugonjwa wa presha ataanzishiwa na matibabu hospitalini kulingana na dawa ipi itafanya kazi kwake haraka, gharama za dawa, na magonjwa yaliyoambatana na ugonjwa wake wa presha.

matibabu haya huanzishwa hospitali tu na sio kwenye duka la madawa na dawa hizi hupatikana bure kabisa kwenye hospitali za serikali.

Lengo kuu la matibabu ni kuzuia matatizo yatokanayo na presha ya damu mfano wa dawa hizo ni captopril, nifedipine, propanalol, atenolol, na zingine nyingi sana.

virutubisho mbadala; 
mara nyingi presha inapata watu wenye umri mkubwa, yaani zaidi ya miaka 40.uwezo wao kuchukua virutubisho kwenye chakula ilicholiwa hua unapungua na kulingana na ubize wa maisha watu hua hawali mboga za majani hata wakila hawali za kutosha hivyo kiwango cha cholestrol au rehemu hua juu sana na kuzuia presha kushuka kirahisi. virutubisho hivi husaidi mwili kushusha cholestrol mwilini na kupunguza uzito mwilini.kama ifuatavyo...

field of greens;hivi ni virutubisho ambavyo vina mboga za majani nyingi sana ambazo hupunguza kiasi cha cholestrol au lehemu mwilini, kupunguza kiasi cha sukari mwilini kwa wagonjwa wa kisukari,husaidia mzunguko wa damu na kuondoa sumu mwilini. kwa kufanya hivi presha hupungua na kua katika hali ya kawaida lakini pia husaidia kupunguza uzito.

garcinia plus;bidhaa hizi za asili zinapatikana huko bara la asia kwenye miti inaitwa garcinia cambondia na kusindikwa marekani ili zisiharibike kwa matumizi ya binadamu.
inazuia ubadilishaji wa wanga kua mafuta mwilini hivyo kupunguza unene kwa kuyachoma mafuta.
inapunguza sana hamu ya kula na kujisikikia umeshiba muda mwingi na kupunguza uzito na kitambi zaidi na watu wa maeneo haya ya asia hutumia sana mti huu ndio maana ni wembamba.

matumizi; tumia kidonge kimoja saa moja au nusu saa kabla ya kula kutwa mara tatu.hivyo kama nilivyoeleza hapo juu hii itasaidia sana kuweka presha katika hali nzuri.ONYO;virutubisho hivi havikufanyi uache dawa za hospitali kwani hufanya kazi kuzisaidia dawa zile za hospitali kwani kuna watu wanatumia vidonge vya hospitali na presha haishuki hivyo vinatumika kama chakula tu.
                                                                      
Elimu kwa wagonjwa:

  • Ukishagundulika na presha tafadhali usiharibu fedha zako kwa waganga wa kienyeji wanaodai watakuponya kabisa, ugonjwa huu ukishaupata hauponi kabisa ila unaweza kuuweka katika hali nzuri kwa kumeza dawa za na kufuata masharti ya daktari kama nilivyoelekeza hapo juu presha maisha yako yote..


  • Kwa matokeo mazuri presha ya damu haitakusumbua iwapo ukifuata aina zote mbili za matibabu yaani yale ya dawa na yale yasiyo ya dawa.


Mwisho wa ugonjwa wa presha.

  • Watu wengi wanaogunduliwa na ugonjwa huu presha zao zitaendelea kupanda kadri umri unavyozidi kua mkubwa.
  • Ugonjwa huu usipotibiwa na kufuata masharti uwezekano wa kufa ni mkubwa sana ndio maana jina lake lingine ni SILENT KILLER yaani unaua kimya kimya na watu wengi ambao unasikia wamefia bafuni au usingizini wameuawa na ugonjwa huu.
  • Ugonjwa huu unaweza usije na dalili hata moja na kuna watu wengi sana wameshakufa bila kujua kama waliugua presha hivyo ni vizuri kupima presha yako angalau mara mbili au nne kwa mwaka.


Madhara ya mwisho ya ugonjwa wa presha..

  • Kupooza mwili na kushindwa kutembea kitaalamu kama kiharusi au stroke.
  • Figo kushindwa kufanya kazi na kufa.
  • Moyo kushindwa kufanya kazi.
  • Kupofuka kabisa.
  • Kuharibika vibaya kwa mishipa ya damu.
Pia waweza kutumia virutubisho vya Agi Plus na Garlic Thyme kwa ajili ya kuepuka au kuweka presha yako iwe safi muda wote...Piga 062559100
 
Top