Tunda la nanasi lina vitamin C, madini ya chuma na aina zingine za madini. Ni tunda zuri kwa kutibu matatizo ya kukosa au kutokupata choo vizuri (constipation) na tatizo la uyeyushaji wa chakula mwilini (poor digestion). Tunda hili husaidia katika uyeyushaji wa vyakula vya proteins katika miili yetu. Yaani kama unakula chakula chenye protein ni vema ukala na tunda hili wakati wa mlo wako. 

Juisi ya nanasi ambali halijaiva sio nzuri kwa mwanamke mwenye ujauzito kwani huweza kusababisha mimba kutoka (it causes uterine contractions). Kwa kuwa tunda hili lina vitamin C ni tunda zuri kwa ajili ya kusaidia mwili kujenga kinga yake.

Unaweza kutumia nanasi kama tiba ya magonjwa mbalimbali kama ifuatavyo:

  • Tunda nanasi likiliwa husaidia ueyushaji wa chakula mwilini. Kama una tatizo la uyeyushaji hafifu wa chakula (poor digestion) kula tunda hili.
  • Tunda hili likiliwa husaidia kuondoa minyoo katika utumbo.
  • Juisi ya nanasi ambalo halijaiva husaidia kutibu tatizo la kukosa au kufunga choo.
  • Vipande vya nanasi vikiliwa pamoja na chumvi na pilipili husaidia kutibu tatizo la mwili kushindwa kuyeyusha chakula.
  • Kutibu tatizo la mawe kwenye kibofu cha mkojo (kidney stones) kunywa juisi ya nanasi kila siku asubuhi kabla hujala chochote kwa muda wa mwezi mmoja. Watu wengine wamekuwa wakikimbilia hospitalini kufanyiwa operesheni. Hii sio njia nzuri ya kukimbilia kwa sababu operesheni huondoa kiungo cha mwili ambacho kina kazi yake muhimu katika mwili wa binadamu.
 
Top