Wataalamu wa afya wameeleza kuwa kati ya asilimia 17 - 20 ya vifo vya wajawazito nchini husababishwa na kifafa cha mimba.

Daktari wa  Afya ya Jamii, Isack Maro amesema kifafa cha mimba ni miongoni mwa magonjwa yanayowapata wajawazito na kusababisha vifo vingi katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwamo Tanzania.

“Hali hii ambayo kitaalamu hujulikana kama pre-eclampsia, huonekana zaidi wakati wa ujauzito wa kwanza, lakini inaweza kujirudia hata katika ujauzito wa pili.


“Mjamzito huwa na viashiria vitatu ikiwamo uwapo wa shinikizo la juu la damu, kiwango kikubwa cha protini mwilini pamoja na kuvimba miguu au mwili. Vitu hivi ndivyo hutoa bainisho sahihi la kitabibu,” amesema.
 
Top