C2
Upangaji uzazi ni suala nyeti ambalo nia yake ni kuthibiti idadi ya watu nchini na kote ulimwenguni.Mtu mzima ambaye ana uwezo wa kuzaa inafaa azae watoto anaweza kimu mahitaji yao ya kimsingi hadi pale wanaweza kujitegemea  maishani.lakini hili limeonekana kinyume.Kwa mujibu na mila na tamaduni za kiafrika na kasumba ambazo zimepitwa na wakati,zinadokeza kuwa kuzaa watoto wengi ni jambo ambalo linampa mwanamume hadhi katika jamii husika.Swali ambalo tunapaswa kujiuliza ni mbona uzae watoto  ambao huwezi kulea?
C4
Wengi hawajakubali ukweli kuwa kuzaa  si kazi kazi ni kulea.Hivyo kuna haja ya mashirika husika na washika dau katka uthibiti wa idadi ya watu ulimwenguni kujitokeza  na kuwaelimisha wananchi watu wazima njia za kupanga uzazi na idadi  bora ya kupata watoto ili kupunguza idadi ya watoto ambao wametelekezwa na kuishia kurandaranda mijini kuombaomba ili kutia kitu mdomoni.
C1
Motto ni Baraka kutoka kwa maulana hivyo basi hakuna haja kutesa viumbe hivi  visivyo na hatia baada ya kutua duniani na kurambishwa shubiri badala ya asali.
Serikali pia inafaa kubuni mradi wa kufadhili mahitaji ya watoto wawili  kama matibabu,elimu na lishe katika kila familia kusaidia katika kuthibiti hali ya kuzaliwa watoto wengi katika jamii yetu.
 
Top