Mahitaji
1. Maembe
2.sukari
3. Tangawizi
5. Iriki

HATUA

1. Chemsha maji ya kutosha mf lita 2 hadi 5 kulingana na wingi wa matunda

2.chukua matunda yako na uyaoshe vizuri kwa kutumia maji ya vuguvugu yaliyowekwa chumvi kiasi ili kuua vijidudu

3. Menya matunda yako taratiibuuu bila kujikata vidole

4.katakata matunda katika vipande vidogo vidogo ili kuiwezesha blender yako kusaga matunda kwa urahisi.

5.chukua matunda, iriki na tangawizi kisha weka ktk brenda na anza kusaga kwa kasi uipendayo. Unaweza kuongeza maji yaliyochemshwa wakati wa kusaga ili kupata mchanganyiko wa wastani usio mzito sana.

6. Chukua maji yaliyochemshwa changanya na rojo la matunda kwa kiasi kulingana na wingi wa matunda kisha koroga.

7. Chukua chujio safi na chuja mchanganyiko wako huo. 

8. Chukua sukari na uitie katika mchanganyiko wako. Kisha koroga hadi sukari yote iyayuke.

9. Chukua chombo safi maalum kwa kuwekea juice na anza kuitia juice ktk vyombo hivyo mf. Chupa za plastiki

10. Weka juice yako katika friji. Unaweza kunywa juice yako na vitafunwa mbalimbali unavyopenda
 
Top