Saratani imeendelea kuwa tishio Tanzania na sasa
unaambiwa saratani ambazo zilikuwa hazijawahi kujitokeza au kuonekana
kipindi kilichopita, sasa ndio kama zimezaliwa na watu mbalimbali
Tanzania wanakutwa nazo.
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga kutoka taasisi ya Saratani Ocean road Julius Shija amekaa na millardayo.com na kusema takwimu zinaonyesha kuwepo kwa saratani ya mdomo na koo kwa kiasi kikubwa kuliko miaka iliyopita Tanzania.
Kwenye sentensi ya pili akasema >>> ‘Watanzania wasipende
kuiga mambo ambayo si sahihi bila kujua madhara yake kama kufanya
mapenzi kwa kuhusisha mdomo, saratani ya mdomo ipo na nyingine
zinasababishwa na zinaa’
Anasema kwenye kupokea wagonjwa wapya kila siku kwenye taasisi hiyo,
Wagonjwa waliopata saratani hiyo mdomoni na kwenye njia ya juu ya hewa
baada ya kujamiiana kwa njia ya mdomo wanaongezeka na sasa wanapokea
Wagonjwa 500 mpaka 600 tofauti na kipindi cha miaka ya tisini mwishoni
na miaka ya elfu mbili mwanzoni walipokua wakipokea Wagonjwa 200-300.
Kwa kumalizia anasema virusi hivi kikawaida vinakuwa kwenye sehemu za
siri na vinasambaa kwa njia ya kujamiiana na vinasababisha baadhi ya
saratani kwenye sehemu za siri kwa mfano saratani ya shingo ya uzazi kwa
Wanawake.