Utafiti
uliochapishwa na jarida la Microbiome la Uingereza limeonyesha kuwa
upigaji busu unaweza kusafirisha zaidi ya bakteria milioni80 kutoka kwa
mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Daktari
Sophianis Nyomyani wa Hospitali ya Mwananyamala anazungumzia utafiti
huo na kusema bakteria wengi ambao huambukizwa kwa njia ya busu na
wengi huchukulia busu kama njia pekee ya kuonyesha upendo.
Utafiti
huo pia umesema wapenzi ambao hupigana mabusu kwa wastani wa mara tisa
kwa siku huwa na bakteria ambao wanaendana na hubadilishana kila
wanapofanya tendo hilo.
“Ni
upendo ila kiafya si salama,hata kama wanandoa wanashiriki katika
kupigana busu,isiwe kwa kila mtu,ni lazima kuwe na mipaka,unaweza
kumbusu mtu shavuni,nje ya mdomo,mkononi na kwingineko lakini siyo
lazima mdomoni.