Tumekuwa tukichambua matatizo ya fangasi sehemu za siri na leo
tunamalizia kueleza vipimo ambavyo mgonjwa anaweza kufanyiwa na tiba ya
tatizo hili. Endelea...
Uchafu unaotoka sehemu za siri huchunguzwa kwa kutumia darubini yaani
microscope baada ya kuchukua sehemu ya uchafu kwa kutumia swab (vijiti
maalum), kipimo hicho humwagiwa tone la 10% potassium hydroxide ambayo
huyeyusha chembechembe za ngozi na kubakiza seli za Candida albicans.
Mgonjwa anaweza kufanyiwa vipimo vya mkojo yaani urinalysis na
kuangaliwa kama ana dalili za magonjwa mengine kama ya kisukari,
HIV/AIDS, ugonjwa wa kuvimba tezi la koo au saratani ya tezi ya koo
yaani thyroid cancer nk.
TIBA
Fangasi hutibika vizuri na mgonjwa kupona ila ni vizuri akaenda
hospitali na kufanyiwa kipimo cha mkojo ambapo chembechembe za yeast
huonwa vizuri kwenye darubini.Daktari akigundua mgonjwa ana maradhi haya
ataweza kumpa dawa zenye uhakika. Usinunue dawa hovyo na kutumia
utasababisha usugu wa fangasi, hivyo kutopona.
Mgonjwa ahakikishe sehemu iliyoathirika inakuwa kavu masaa 24 na apake
poda yoyote ya kutibu fangasi asubuhi na usiku kwa wiki 4
mfululizo.Mgonjwa, kwa ushauri wa daktari atameza dawa za antibayotiki
kama vile cloxacillin 250mg (2 x 3 siku 5) kama sehemu yenyewe imekuwa
na kidonda ili iweze kukausha haraka, anashauriwa asivae chupi bali avae
bukta yenye kuruhusu hewa kupita na ajikaushe vizuri baada ya kuoga.
USHAURI
Ushauri pia unatolewa kwa mgonjwa asitumie sabuni zenye dawa kwani
zitamsaidia kwa muda lakini zitafanya ngozi kupoteza uwezo wake wa asili
wa kujilinda dhidi ya vijidudu na ahakikishe anabadili nguo ya ndani
kila siku na iwe safi iliyopigwa pasi.
Kwa ushauri wa daktari mgonjwa anaweza kutumia ‘cream’ iliyo kwenye
tyubu inayoitwa Quadrimerm au fluocinonide cream kwa wiki mbili kwa
kupaka sehemu iliyoathirika ikiwa kavu na akae dakika 30 kabla ya kuvaa
nguo.
Pia nakushauri ununue co-trimazole powder uwe unatumia wakati ukienda kazini jinyunyizie hasa kwenye maungano ya mapaja.