Huenda umekuwa ukipata shida kutambua ni wakati gani upo katika hatari ya kupata ujauzito au la!.
Leo nakupa hizi alama au dalili zinazoashiria kuwa mwili wako (mwanamke) upo katika ovulation.
Ovulation ni ile hali ya kutoka kwa yai la kike baada ya kukua na kukomaa katika ovary.
Kimsingi kuna alama au viashiria ambavyo huashiria ovulation, hivyo hali hiyo huweza kukusaidia kupanga siku maalum ya kujamiana kwa ajili ya kupata mimba.
Alama hizo zipo nyingi, lakini leo nitakwambia hizi chache kama ifuatavyo;
Mwanamke hujikuta akipata ongezeko la matamanio ya kujamiana, hiyo hutokea siku chache kabla ya kufika wakati wa ovulation, ambao ni wakati mzuri zaidi wa kujamiana iwapo unataka kubeba mimba.
Ishara nyingine ni kuhisi maumivu katika matiti, hii ni kwa baadhi ya wanawake hujihisi kupata maumivu haya wakati wanapokaribia ovulation au mara baada hapo.
Jambo hili huusiana sana na mabadiliko ya homoni mwilini ambazo hujitayarisha kwa ajili ya kubeba mimba.
Hata hivyo, ishara hii si maalum sana kwani kuna baadhi ya wanawake hupata maumivu kwenye matiti kabla ya hedhi.
Dalili nyingine au kiashiria kingine ni kupanda kwa joto la mwili, ongezeko la joto la mwili husababishwa na progesterone ambayo huongezeka sana mara baada ya ovulatio.