Uhali gani mpendwa msomaji wa www.dkmandai.com, napenda kuwashukuru wale wote ambao wameendelea kuuliza maswali yao kupitia namba zetu za Mandai Herbalist Clinic yaani zile za 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800.

Baada ya shukrani hizo kwa sasa naomba nitumie fursa hii kujibu swali lililoulizwa na wadau wetu wa tovuti hii waliopenda kujua kuhusu maana ya ugumba na tofauti kati ya mtu mgumba na tasa.

Tukianza na ugumba hii ni ile hali ya kutoweza kupata ujauzito katika kipindi cha mwaka mmoja au zaidi kwa wenzi ambao wamekuwa wakifanya mapenzi bila kutumia njia zozote za uzazi wa mpango.

Hali hiyo huweza kutokea kutokana na tatizo kwa mwanaume au mwanamke, licha ya kwamba asilimia kubwa ya watu wamekuwa wakidhani wanawake peke yao ndio ambao hupata tatizo hilo. Hivyo ni vyema ikafahamika kuwa tatizo hili huweza kuwa kwa mwanaume au mwanamke na ni tatizo ambalo linatibika na kuisha.


Baada ya kufahamu hayo kuhusu ugumba sasa tufahamu tofauti iliyopo kati ya Ugumba na Utasa
 

Utasa ni ile hali ya mwanamke kutoweza kushika ujauzito kabisa au mwanaume kutoweza kusababisha ujauzito kwa mwanamke kabisa.

Katika hili utofauti wake unakuja hivi mtu tasa huwa anakuwa hana uwezo wa kupata mimba kabisa au kumpatia mwenzi wake mimba kabisa, lakini kwa mtu mgumba yeye huwa anakuwa na uwezo wa kuja kupata mimba iwapo tatizo lake litapatiwa ufumbuzi.
 
Top