Wanawake wengi wanapokuwa na ujauzito huwa wanaomba Mungu awasaidie waweze kujifungua salama, ingawaje kujifungua nakohuwa na changamoto zake kwani kuna wakati huweza kujifungua kwa upasuaji jambo ambalo huogopwa na kinamama wengi.

Lakini hata hivyo kujifungua kwa njia ya kawaida  nako huwa kuna kashi kashi zake  kidogo, hasa maumivu ya uchungu. 

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo mwanamke huweza kukabiliana nayo mara baada ya kujifungua kwa njia ya kawaida, ingawa sio lazima upate yote.

Mara baada ya kujifungua mama huweza kupata baadhi ya michubuko sehemu zake za uzazi na hivyo michubuki hiyo husababisha maumivu kwa mama au wakati mwingine njia inabidi iongezwe kwa kuchanwa. Jambo ambalo huchangia maumivu baada ya kujifungua licha ya kuwa yatakuwa yakipungua kadri siku zinavyoenda.

Pia mama huweza kupata maumivu wakati wa kupata choo, hivyo hushauriwa mama kupendelea kutumia vyakula vyenye kambakamba 'fiber'  na matunda pamoja na kuzingatia kunywa maji mengi ili kusaidia kuweka sawa mfumo wa umeng'enyaji wa chakula tumboni na kukusaidia kupata choo  laini.

Baada ya kujifungua mama huweza kuwa akipatwa na maumivu ya tumbo, maumivu hayo huchangiwa na misuli ya tumbo la uzazi kusinyaa, lakini ukiona maumivu yanaongezeka unaweza kufanya jitihada za kuonana na daktari kwa uchunguzi zaidi.
 
Top