Mzizi wa papai |
Papai kama tunda tayari tumeshalizungumza mara kadhaa sasa, hivyo nimeona kwa sasa ni wakati mzuri wa kuhamia upande wa miziz ya mmea wenyewe.
Mizizi ya mpapai inapochemshwa huwa na uwezo mzuri wa kumsaidia mgonjwa mwenye shida ya mawe kwenye figo, ambapo mgonjwa atapaswa kuchemsha mizizi hiyo kisha kusubiri yapoe halafu atakunywa nusu kikombe asubuhi na jioni kila siku.
Aidha, mizizi ya papai pia ina sifa ya kutuliza maumivu ya kibofu cha mkojo, ambapo mhusika atatakiwa kupata mchemsho wa miziz hiyo kisha takunywa kama ilivyoainishwa hapo juu.
Pia mizizi hiyo ya papai inaelezwa kuwa ni msaada mkubwa wa kuondosha maambukizi katika njia ya mkojo. Katika hii nayo mhusika atakunywa mizizi kama ilivyoainishwa hapa juu.
Majani ya mpapai |