Moja ya matatizo ambayo huleta huzuni na uchungu ndani ya familia ni pamoja na hili swala la familia kushindwa kubahatika kupata watoto.
Hali hiyo hupelekea huzuni ndani ya nyumbana, chuki, lawama, kejeli na kushutumiana na kusababisha hata talaka pia kati ya wanandoa
Lakini leo nimeona nianze kuzungumzia hili tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi jambo ambalo mwishowe hupelekea ugumu wa mama kushika ujauzito.
Matatizo ya kuziba mirija hutokea pale mwanamke anapopata maambukizi ya mara kwa mara ukeni yanayoambatana na muwasho kutokwa na uchafu na usaha ukeni, maumivu wakati wa tendo la ndoa na kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa.
Maambukizi hayo huwa na nafasi kubwa ya kusababisha mirija kuziba na ikiwa nje ya mirija husababisha mirija kujikunja.
Maambukizi haya yasipotibiwa kikamilifu huenea hadi katika mfuko wa uzazi na kushambulia tabaka la ndani la kizazi na kusababisha tatizo liitwalo ‘Endometriosis’ ambapo mwanamke hulalamika maumivu ya chini ya tumbo au chini ya kitovu mara kwa mara, kutokwa na uchafu ukeni na dalili nyingine zenye kufanana na hizo.

Dalili ambazo huashiria mwanamke tayari amepatwa na tatizo hili la mirija kuziba ni pamoja na mwanamke kutafuta ujauzito kipindi kirefu bila mafanikio.
Pia mwanamke mwenye shida hii mara nyingi huwa na kawaidia ya kupatwa na maumivu chini ya tumbo kwa muda mrefu.
Dalili nyingine ni kuharibika kwa mimba mara kwa mara au kuzaa mtoto mmoja kisha unapotafuta mwingine huwa inakuwa ni kazi ngumu kumpata tena