Kutokwa damu kipindi cha ujauzito ni hali hatarishi , inawezekana ni dalili ya kutaka kuharibika kwa mimba au complications za mimba tu, mama atokwa damu kwa kiasi kidogo(matone) au kiasi kikubwa,haswa kipindi cha miezi 3 ya kwanza ya mimba  (first trimester) mpaka miezi 3 ya mwisho( third trimester )

pregnant


Damu inapotoka kiasi kidogo cha matone (spotting) hapo inaweza matatizo kama ya infection au dalili ya kuharibika kwa mimba ,ila damu inapotoka kwa wingi hiyo inakuwa hali nyingine kabsa ,complication nyingine zinazoweza sababisha mama kubleed damu kwa wingi

                            :Kuharibika kwa mimba

                            :Kuharibika kwa placenta

                        :Yai kutungwa nje ya mji wa mimba (ectopic preganancy)

                            : Kondo (placenta) kuwa na matatizo kwenye ukuta wa uzazi

Mama anapotokwa damu huambatana na maumivu  chini ya tumbo ,kizunguzungu ,kushindwa kuona vizuri na kuishiwa nguvu.



phototake_photo_of_8_week_fetus_circle

Takwimu zinaonyesha kwa asilimia 25 ya wamama wajawazito wanatokwa na damu kipindi cha miezi 3 Yao ya mwanzo (first trimester). Mimba inapotungwa inapofika wiki ya 4 yai linakuwa fertilized na kushikilia uterine wall , hiyo hali inaweza msababishia mama kupata damu nyepesi  kwa muda na baadae itakata(implantation bleeding).



imagesDN9KZGFP
implantation bleeding inakuwa hivi, damu nyepesi yenye kibonge







 : Mabadiliko ya mwili yanachochewa na homoni (hormonal changes),inasababisha mama kutokwa damu matone madogo madogo (spotting)



  :Kushiriki tendo la ndoa uume akigonga kwenye mlango wa uzazi kunaweza msababisha mama kutokwa damu kidogo (matone),mama akiona iyo hali ni vizuri kuachaa  kushiriki tendo la ndoa muda kwanza.





  :Infections-maambukizi yanapompata  kupitia ukeni au cervix  kama  U.T.I,kaswende,gonorea n.k ni rahisi kutokwa damu kipindi cha miezi 3 ya kwanza (first trimester).Mama mwenye infections anatakiwa kuwahi hospital ili kuokoa maisha yake na mtoto, infetions husababisha watoto kuzaliwa na ulemavu (kuona,kusikia n.k)



 phototake_photo_of_8_week_fetus_circle


  :Mama anapofanyiwa vipimo na mkunga au daktari  na kuwekea kidole ndani ya uke kunaweza msababishia kutokwa damu matone .

26113tn
internal exam

 : Kuharibika kwa mimba(miscarriage)mjamzito hutokwa damu kwa wingi yenye madonge makubwa au madogo kidogo iiyo ni ishara kubwa ya kuharibika kwa mimba

  :Mimba inapotungwa nje ya mfuko wa uzazi na badala yake inakuja kutungwa kwenye mirija ya uzazi(fallopian tube) hapo nafasi ya kulea mimba na kukuzia mpaka miezi 9 ni ndogo ,hiyo hali inamletea mama kupata damu kwa wingi ,ndio mana wizara ya afya inashauri mama unapopata mimba toa taarifa kituo cha afya usisubirie ikue miezi 4-5 ndio uanze clinic.

  :Matatizo ya kondo (placenta) inapoharibika,kunachangia mama kutokwa damu

  :Mama anapojifungua kabla ya week 37 (preterm labor) atasikia kutanuka kwa Uke, kunaweza ambatana na damu ,kuhara,maumivu ya mgongo, na mvuto kwenye nyonga .


imagesDN9KZGFP


USHAURI


Unapoona damu inakutoka haijalishi kidogo au nyingi ,wahi hospital sababu hujui nini kimesababisha na inaweza kuwa dalili ya kuharibika kwa mimba . Kwa matibabu utafanyiwa  ultra sound na vipimo vingine vya ukeni na tumboni n.k kujua tatizo ni nini.
 
Top