Maumivu ya mgongo kwa mama mjamzito ni tatizo la kawaida linalowasumbua wamama wengi .  Husababishwa na mabadiliko ya hormone Kwenye mwili wa mama na kuchochea kupata maumivu ya mgongo .Mtoto anavyozidi kukua na kuongezeka uzito  unaokuja kumuelemea  mama na kupata maumivu ya mgongo.
image


MAMA JIEPUSHE !

1. Epuka kuvaa viatu virefu na badala yake vaa viatu flat .

2. Usitumie mda mrefu kusimama,kukaa au kulala.

3. Usibebe mzigo mzito .

4: Usifanye Kazi nzito.



NJIA YA KUONDOA ️AU  KUPUNGUZA MAUMIVU.

Mama anatakiwa kufanya mazoezi kwa ajili ya afya yake.

1. Fanya mazoezi kila siku ya kutembea asubuhi na jioni kwa mwendo wa dakika 20-35

2. Mazoezi ya kujinyoosha viungo vya mwili mazuri ,yanasaidia muscles za mwili kulegea.

3. Mazoezi ya kuogelea yatakusaidia ila uwe makini na Maji.

4. Jipe mda wa kutosha upumzike ,ulale kwa masaa 10-12 kwa siku.

5 .Massage therapist anaweza kukufanyi massage, kwa kipindi cha siku 5-10 maumivu yakaisha.

image

DALILI HATARISHI

Mama mjamzito utakapo hisi maumivu makali sana yanayo ambatana na maumivu ya miguu,na ni ngumu kupata  haja  ndogo na kubwa kama unavyopata kawaida hapo ujue kuna tatizo wahi  hospital.

Comments
 
Top