Utafiti wa shirika la Afya Duniani (WHO) umebaini kwamba matatizo ya afya ya ndani ya mwanamke na maambukizi ya maradhi ya sehemu za siri kwa wanawake (gynocological disease) yanaongezeka kwa kasi kubwa sana duniani.

Takribani asilimia 85% ya wanawake wanasumbuliwa na matatizo hayo, kati ya hao asilimia
75% ni wanawake wa kiafrika na asilimia 60% kati ya hao hawajajitambua, na wengine
wanajitambua lakini wanapuuzia,au wanakosa wapi wapate msaada.
Sasa tuangalie undani wa mwanamke


Mwanamke kwa kawaida ana sura tatu (3). Je! Unazifahamu?

(i) Sura ya nje (Reception)
Wengi husema mwanamke reception; wanawake wengi hujitahidi kwa gharama zote
kuhakikisha reception yao au muonekano wao wa nje upo safi na salama muda wote.

(ii) Sura ya pili ya mwanamke nyumbani kwake
Muda wote mwanamke huwa anahakikisha nyumbani kwake panakuwa safi na wengine hata kuajiri watu, wanalipwa mshahara kazi yao ni kuhakikisha mazingira hayo ya nyumbani yanakuwa safi mara zote.

(iii) Sura ya tatu ya mwanamke ni sura yake ya ndani, uke wa mwanamke na kizazi
Hii ndiyo sehemu nyeti na muhimu sana kwa mwanamke na ndio sehemu imemfanya

mwanamke aitwe mwanamke na apewe heshima na wanaume na sehemu hiyo pia inatakiwa kuwa safi na kutazamwa muda wote. Lakini fikiria eneo hili wanawake wengi hawalithamini wala kulipa kipaumbele, na

ndio sababu imepelekea kusababisha matatizo makubwa ya kiafya katika eneo hilo.
Hebu jiulize swali; kama kweli kila siku unaweza kujicheki kwenye kioo mara kadhaa
kuhakikisha reception yako ya nje iko safi, na kila siku unafanya usafi nyumbani kwako
kuhakikisha mazingira ya nyumbani kwako ni safi na salama.

Je! Ni marangapi au ni lini umeweza kucheki afya yako ya ndani kwa mara ya mwisho au ni mara ngapi kwa mwaka unakwenda hospitali kucheki afya yako ya ndani? Au kucheki afya yako ya kizazi? Fahamu ya

kwamba maradhi yoyote kuanza taratibu na ukua kadri siku zinavyokwenda Utakubaliana na mimi kwamba eneo hilo muhimu na nyeti halijathaminiwa kwa wanawake walio wengi.
Utafiti umebaini baadhi ya vyanzo vikuu vinavyoweza kusababisha maambukizi ya maradhi ya sehemu za siri kwa wanawake wengi ni;

i) Vyoo vya kuchangia (public toilets)
Eneo hili ni hatari sana katika kusababisha maambukizi.kwa hiyo unahitaji kuwa
mwangalifu sana sehemu yoyote yenye mikusanyiko ya watu ambayo itawalazimu
(kuchangia vyoo kama; maofisini, maeneo ya soko, nyumba za ibada , sehemu za starehe,kwenye nyumba zetu tunakoishi nyumba za kupanga,vyuoni,mashuleni, nk...

(ii) Kutotumia maji safi na salama.
Maji mengi tunayotumia sio safi na salama mengi yana bacterias. Wengine eti hujazia maji ndani ya ndoo halafu huwekwa chooni. Maji hayo huhifadhi bacterias ni hatari sana.

(iii) Matumizi ya pads za hedhi ambazo sio salama.
Utafiti pia umebaini wanawake wengi wanapomaliza hedhi huanza kutibu fangasi, wengine hupata michubuko, miunguzo, miwasho na vipele sehemu za siri. Kwasababu tu wametumia pads ambazo sio salama.

(iv) Bacterias
Bacteria hupatikana sehemu mbalimbali na katika mazingira mbalimbali, unahitaji umakini katika matumizi ya vitu ktk sehemu za ndani.

Pia unapofua nguo yako ya ndani unashauriwa kupiga pasi kabla ya kuvaa. Swali, ni wanawake wangapi wanapiga pasi nguo zao za ndani kabla ya kuvaa?
Vyanzo ni vingi sana, suluhisho ni nini? “Kinga ni bora kuliko tiba “ ni vyema ukafahamu
namna ya kumdhibiti muhalifu kabla hajaingia ndani kwako kuliko kupambana nae akiwa
tayari ndani ni ngumu. Ndo maana tumejitoa kuelimisha na kukushauri, jinsi ya kupambana na adui kabla na hata kama atakuwa ameingia kujua jinsi ya kumshinda.
 
Top