MZUNGUKO WA HEDHI NI MZUNGUKO WA KILA MWEZI AMBAO HULETA KUTOKWA NA DAMU UKENI KUTOKANA NA MIMBA KUTOTUNGWA. KWA KAWAIDA HEDHI YA KWANZA HUTOKEA KATIKA UMRI  WA  MIAKA 12 -13. MZUNGUKO HUU WA HEDHI HUWA UNADHIBITIWA NA HOMONI ZINAZOZALISHWA NA MWILI. HEDHI HUTOKEA PALE AMBAPO TISHU ZA UKUTA WA MJI WA MIMBA UNABOMOKA NA KUTOKA KAMA DAMU UKENI.

Kila mwezi ovari za mwanamke huzalisha yai moja la uzazi. Yai hili huweza kukaa kwa muda mpaka wa masaa 36 ndani ya mirija na tumbo la uzazi. Inapotokea yai hili halijarutubiwa, ukuta wa mji wa uzazi hubomoka na kutoka kwa njia ya uke pamoja na damu. Hali hii huitwa hedhi.
Mzunguko wa hedhi huanza kuhesabiwa siku ya kwanza mwanamke anapoanza kupata siku zake.

Urefu wa Mzunguko wa hedhi

Mzunguko wa hedhi huwa na siku 21 mpaka 35, zaidi au chini ya hapo huashiria tatizo. Mwanamke huwa katika hedhi kwa wastani wa siku 3 -7, zikizidi zaidi ya siku 7 kwenye hedhi huweza kuashiria tatizo.
Namna mzunguko wa hedhi ulivyo

katika mfano huu tutachukulia mzunguko wenye wastani wa siku 28.
Siku ya 1 mpaka 5 ni kipindi ambacho mwanamke anaingia kwenye hedhi yake, huu ni mwanzo wa mzunguko wa hedhi. Kipindi hiki ukuta wa mji wa mimba hubomoka na kutoka pamoja na damu ukeni kama damu ya hedhi. Homoni za istrojeni na projesteroni huwa zimepungua.
Kipindi kinachofuta cha siku ya 6 mpaka 14 huwa ni kipindi ambacho ukuta wa mji wa uzazi huanza kujengwa tena kuundaa kwa ajili ya kupokea kiini tete. homoni ya istrojeni huwa kwa wingi na hudhiti shughuli hii.
Yai la uzazi huzalishwa (Ovulation) siku ya 14 ya mzunguko, na huweza kukaa kwa masaa 36. yai hili hutoka kwenye ovari na kusafiri kwenye mrija wa uzazi.
Kipindi kinachofuata cha siku ya 15 mpaka 28 homoni ya projesteroni huzalishwa kwa wingi na kazi yake huwa ni kuutunza ukuta wa mji wa mimba.
Ikitokea yai la uzazi halijarutubiwa na mbegu za kiume, homoni ya projesteroni hupungua mwishoni mwa mzunguko. Kupungua kwa homoni hii husababisha ukuta wa mji wa mimba kuanza kubomoka, hali hii husababisha kutoka kwa damu ukeni na kuashiria kuanza kwa mzunguko mwingine wa hedhi.
Kiasi cha damu katika hedhi

Kwa kawaida katika hedhi damu inayotoka huwa na rangi ya  na huwa haina mabonge. Kiasi cha damu kinachopotea kwa njia hii ni mililita 35 mpaka 50 kwa siku. Ni sawa na kutumia pedi 2 ambazo hazijaloa damu kabisa.
Siku salama na Siku za hatari.

Watu wengi hupenda kujua siku salama ambazo mwanamke hawezi kupata ujauzito au hatari ambazo mwanamke anaweza kupata ujauzito. Unaweza kuzijua siku salama kama mzunguko wa mwanamke haubadiliki.
 Matatizo yanayoambatana na hedhi

Kuuna hali mbalimbali zinazoweza kumbatana na hedhi, bofya kwenye mada ili ujifunze zaidi.
Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi
Premenstrual syndrome
Kupata hedhi kwa muda mrefu zaidi
Damu kuwa na mabonge
Kukosa hedhi
 
Top