Napenda kuchukua nafasi hii kujibu swali la pili la mdau mmojawapo wa Kona ya Afya ambaye ameuliza kuwa, ni vipi anaweza kubeba mimba ya mtoto wa kike. Katika kujibu swali hilo naweza kusema kwamba, ndugu mdau ulimwengu hivi sasa umeendelea sana kiasi kwamba matatizo mengi katika jamii yanatatuliwa kwa msaada wa wataalamu mbalimbali. Mojawapo ni suala la mtu kuzaa mtoto wa kike au wa kiume. Ingawa njia hizo nitakazoziandika hapa pengine hazina uhakika mia kwa mia, lakini wapo watu wengi wamejaribu na zimewasaidia. Hivyo nina matumaini kwa kufuata maelekezo haya ukaweza kupanga na kuzaa mtoto wa kike kama unavyokusudia. Ninachotaka kusisitiza hapa ni kuwa, maendeleo ya elimu hasa katika uwanja wa sayansi na tiba yamekuwa na taathira nyingi katika kupunguza matatizo ya familia kama vile ugumba, kuzaa mtoto wa jinsia inayotakiwa na wazazi, magonjwa ya wanawake, vifo vya wajawazito na kadhalika. Ni ukweli usiopingika kwamba ingawa watu wengi wanazingatia kuzaa mtoto aliye mzima wa mwili na afya bila kujali jinsia ya mtoto huyo, lakini uchunguzi unaonyesha kwamba kuna baadhi ya watu au wazazi wanaopenda kuwa na watoto wa jinsia fulani zaidi. Vilevile imeonekana kuwa wanawake hupendelea kuwa na watoto wa kike huku wanaume wakipenda kuwa na watoto wa kiume. Hata hivyo wazazi ambao tayari wana watoto wa jinsia ya kike au ya kiume hupendelea kuwa na mtoto wa njinsia nyingineyo ili kuwa na watoto wa kiume na wa kike.

Je, ni vipi jinsia ya mtoto huainishwa?
Kinyume na wengi wanavyofikiria kwamba mwanamke au mwili wa mwanamke ndio mwenye jukumu la kuainisha jinsia ya mtoto kwa kuwa yeye ndiye anayebeba mimba, uhakika wa mambo ni kuwa mwanamume ndie mwenye uwezo wa kuainisha jinsia. Kila yai la mwanamke lina chromozu mbili za X. Iwapo manii ya mwanamume au spemu (ambayo in chromozomu X na Y) itakuwa na X na kurutubisha yai la mwanamke lenye X tupu, basi mtoto atakayezaliwa atakuwa mwanamke. Vilevile iwapo spemu ya mwanamume itakuwa na Y na kurutubisha yai la mwanamke, basi mtoto atakayezaliwa atakuwa mwanamume. Hivyo kwa kufahamu suala hilo, ni matumaini yetu kuwa vile visa vya kinamama kuachwa eti kwa kuwa hawakuzaa watoto wa kiume au wa kike vitapungua katika jamii zetu. Mke wako asipozaa mtoto wa jinsia uitakayo, usifikiri kuwa yeye ndio mwenye makosa.
Wakati mwanamume anapomwaga shahawa, spemu kati ya milioni 200 hadi 400 humwagwa katika uke wa mwanamke. Baadhi ya spemu hizo huwa zina chromozomu X na baadhi zina chromozomu Y. Hata hivyo, ni spemu moja tu ambayo hutakiwa kwa ajili ya kurutubisha yai la mwanamke na kuunda mimba. Nadharia mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kusaidia kuchagua ni jinsia gani unaitaka awe nayo mwanao, zinategemea suala la kuandaa mazingira katika uke na mwili wa mwanamume na mwanamke, yatakayosaidia spemu ya baba yenye chromozomu inayotakiwa irutubishe yai la mama, na hivyo kutungwa mimba ya jinsia inayotakiwa.
Njia ya Dr. Shettles ya kuzaa mtoto wa kike
Njia hii imekuwa ikitumiwa na watu wengi kwa miaka mingi sana na imewasaidia kuweza kuzaa mtoto wa kike. Wengi wanasema kuwa uwezekano wa kufanikiwa njia hii ni asilimia 90. Njia ya Dr. Shettles inategemea msingi kwamba, chromozomu Y (yenye kuwezesha kutungwa mimba ya mtoto wa kiume) ni ndogo na yenye kwenda kwa kasi zaidi ikilinganishwa na chromozomu X (yenye kuwezesha kutungwa mimba ya mtoto wa kike) ambayo ni kubwa na huenda polepole. Pia kwa kutegemea kuwa chromozomu X inaishi muda mrefu zaidi kuliko ile ya Y. Hivyo Dr. Shettles anashauri kuwa iwapo unataka kuzaa mtoto wa kike uhakikishe kuwa:
• Unajamiiana siku 2 au 3 kabla ya Ovulation. Kinadharia spemu za kiume zitakuwa zimeshakufa hadi kufikia siku hasa ya Ovulation na kuziacha spemu za kike zikiwa hai tayari kurutubisha yai na kuunda mtoto wa kike.
• Anashauri pia wanawake wajizuie kufikia kileleni (orgasm) kwani hali hiyo itaufanya uke uwe na hali ya asidi ambayo ni kwa faida ya spemu ya kike yenye chromozomu X.
• Pia anawashauri wazazi wanapojamiina wawe katika hali ya mwanamke kulala chini na mwanamume juu au missionary position. Kwani anasema kuwa mtindo huo huziwezesha spemu zenye chromozamu X zimwagike karibu na mlango wa uke na kuwa na uwezekano mkubwa wa kuingia ukeni na kutungwa mimba.
Njia ya O+12
Njia hii inayomaanisha Ovulation jumlisha siku 12 ilivumbuliwa na mama mmoja wa Australia aliyekuwa akihangaika kupata mtoto wa kike baada ya kuzaa watoto 6 wa kiume. Mama huyo anawahusia wale wanaotaka kubeba mimba ya mtoto wa kike wajamiiane masaa 12 baada ya Ovulation. Mama huyo alifuata njia ya Dr. Shettles bila mafanikio katika mimba zake za nyuma. Lakini baada ya kugundua njia yake hii mwenyewe mwishowe alibeba mimba na kujifungua mtoto wa kike.



Kuna wengine wanaamini kwamba baadhi ya lishe na vyakula vya aina mbalimbali husaidia kutunga mimba ya mtoto wa kike. Kwa mfano kuna wanaoamini kuwa kula baadhi ya vyakula huufanya uke uwe na hali ya asidi ambayo husaidia Chromozomu Y ife katika uke. Nadharia nyingineyo inayotumiwa katika kuchagua jinsia ya mtoto inasema kwamba, mwanamke anayetaka kubeba mimba ya mtoto wa kike ale vidonge vya virutubisho (supplements) vya Calcium na Magnessium mwezi mmoja kabla ya kubebea mimba. Iwapo unataka kutumia vidonge vya virutubisho ili uweze beba mimba ya mtoto wa kike, ni bora ushauriane na daktari wako kwanza. Hii ni kwa sababu dawa hizo huweza kuingiliana na dawa nyinginezo za magonjwa mbalimbali.
Baadhi ya vyakula vinavyotajwa kuwa vinasaidia katika kutunga mimba ya mtoto wa kike ni.
• Mahindi, nyama, maharagwe, samaki, tunda damu, mayai na maini.

Vyakula hivyo ni vya asidi hivyo huifanya PH ya mwili wako hupungua na kuwa ya acidi. Hali hiyo husaidia kuua spemu za Y na hivyo kusaidia kuzifanya spemu za X ziwe na uwezekano mkubwa wa kurutubisha yai. Hivyo mwanamke anayependelea kubebea mimba ya mtoto wa kike anashauriwa kutokula vyakula vyenye alikali ambavyo ni kama, ndizi, chokleti, juisi ya machungwa, viazi, tikiti maji na vinginevyo.
Pia sio mbaya kutaja baadhi ya imani na itikadi wanazoamini baadhi ya watu kuwa zinasaidia katika kupata mtoto wa kike:
• Fanya mapenzi wakati wa mchana.
• Fanya mapenzi siku shufwa (even days) za mwezi.
• Fanya mapenzi wakati mwezi umekamilika ( full moon days).
• Kula samaki na mboga mboga kwa wingi, na baadaye kufuatiwa na kitinda mlo cha chokleti.
• M-surprise mwenzi wako, kuna wahenga wanaamini wanawake wanaoanzisha wao kufanya mapenzi huzaa watoto wa kike!]
Hivyo kila la kheri wadau, unaweza kuchagua moja ya njia kati ya zilizotajwa hapo juu na kwa kufuata maelekezo ukajaaliwa kuzaa mtoto wa kike.
 
Top