KUJAMIIANA NA WANAUME AMBAO HAWAJATAILIWA KUNASABABISHA MAAMBUKIZI YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
SARATANI ya shingo ya kizazi inaongoza kwa wingi hapa nchini ikilinganishwa na saratani nyingine ambapo wanawake wenye umri wa miaka kati ya 25 na 50 ndio huathirika zaidi
Saratani hii inachangia kwa asilimia 60 ya aina zote za wagonjwa wa saratani wanaofika kutibiwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam. Hata hivyo utafiti wa kitabibu unaonesha kuwa ugonjwa huu si tu kama unawezekana kutibika na kupona kabisa iwapo wagonjwa wataweza kuwahi kufika hospitali bali hata unaweza kuzuilika kwa kutumia chanjo.
Saratani ya shingo ya kizazi ni mabadiliko ya chembe chembe hai zilizo juu au zinazofanana na shingo ya uzazi ambapo huchukua miaka mingi hadi kujitokeza kwake.
Ugonjwa huu huchukua zaidi ya miaka 15 mpaka 20 kugundulika lakini kabla ya kujitokeza bayana hutokea mabadiliko kadhaa yanayoweza kugundulika mapema na kufanikiwa kuzuilika katika hatua za mwanzoni.
Utafiti uliofanywa na timu ya wataalamu wa ugonjwa huo umebainisha mabadiliko ambayo hujitokeza kabla ya maradhi haya kujitokeza ambapo sehemu ya kizazi kabla ya kujitokeza saratani iitwayo kitaalamu( Pre cancerous lesion) ambapo mabadiko hayo yanaweza kuendelea na kujirudia na kuwa ugonjwa au usiwepo inategemeana na hali yenyewe.
Akizungumza na Blog hii, Mkunga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili ambaye pia ni mchunguzi wa upimaji wa ugonjwa huo kwa akina mama Bi. Matrida Maina, alisema kuwa Saratani ya Shingo ya kizazi inakua kila siku ambapo asilimia 40 ya wanawake hulazwa katika taasisi ya Ocean Road kutokana na ugonjwa huo.
Bi. Matrida alibainisha kuwa uchunguzi uligundua kuwa saratani hiyo ya shingo ya kizazi husababishwa kwa kuanza kujamiiana mapema hasa chini ya umri wa miaka 18, kuwa na wapenzi wengi kujamiana na mwanaume ambaye hajatailiwa ‘mkono wa sweta’kubeba mimba mingi pamoja na kuvuta sigara.
Hata hivyo unywaji wa pombe kupindukia pia nao imeanishwa kuwa ni mojawapo ya mambo yanayochangia kupata saratani ya shingo ya kizazi ambapo pia watu walioathirika na virusi vinavyopatikana kutokana na vitendo vya kujamiiana na UKIMWI wako katika hatarini zaidi kupata maradhi hayo.