Mambo 6 yanayofanywa kila siku ambayo huathiri afyaMambo 6 yanayofanywa kila siku ambayo huathiri afyani yafuatayo:

1. Kukaa kwa muda mrefu

Kwa wakati flani, wote hutumia muda wetu tukikodolea macho kompyuta. Tafiti zinaonyesha kuwa kukaa kwa muda mrefu kunasababisha matatizo ya maradhi ya moyo, kisukari, sonona (depression) na aina nyingine za maradhi ya saratani.

Jambo ambalo wengi wetu hatulijui ni kwamba hata tukiwa tunafanya mazoezi hakuwezi kubadilisha madhara hayo ya kukaa kitako kwa saa nane.

Utafiti huo uliofanywa kwa miaka 12 kwa raia wa Kanada 17,000 kwenye kituo cha Pennington Biomedical Reasearch kilidhihirisha kuwa bila kujali rika, mwili, uzito, au kiwango cha mazoezi, watu wanaotumia muda mwingi kukaa wana muda mfupi wa kuishi.

2. Uvaaji wa viatu, sidiria zinazobana na ubebaji vibegi vya mikononi (Handbags) vizito

Wanawake wanaopambana na maumivu ya sidiria zinazowabana, begi ndogo za mikononi au viatu kwa lengo la kuendana na mitindo mipya, huenda wakafikiri kuwa wanafanya hivyo mkwa wakati huo, la hasha, kwani wataalamu wa afya wanasema hali hiyo ya kutotulizana inaweza kuwasababishia matatizo ya mgongo kwa muda mrefu.

Pembeni mwa mgongo, uvaaji wa sidiria za zinazobana pia husababisha vipele kwenye ngozi, na maradhi mengine, hivyo wanashauriwa kutobeba vitu vizito kwenye mabega yao.

Kituo cha American Chiropractic Association kinapendekeza kuwa wanawake hawapaswi kubeba vitu vyenye uzito wa asilimia 10 ya miili yao kwa kipindi fulani endelevu. Viatu virefu via vimetajwa kusababisha tatizo hilo la mgongo.

3. Matumizi ya simu za kisasa (smartphones) kwa muda mrefu

Hatuwezi kufikiria kuwa tunasababisha madhara makubwa kwa kutumia muda mrefu kwenye simu zetu za kisasa (smartphone au tablet), hasa kwa vijana waliochini ya umri wa miaka 24 ambao hawawezi kugeuza macho yao mbali na simu zao hata kwa sekunde moja.

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na kituo cha Afya cha Uingereza cha Simpyhealth kimedhihirisha kuwa asilimia 84 ya watu waliofanyiwa utafiti wenye umri kati ya miaka 18 na 24 walikuwa wakisumbuliwa na maumivu ya mgongo yanasobabishwa na matumizi ya simu, kompyuta na vifaa vingine vya umeme kwa muda mrefu hasa wanapolala.

Utafiti huo umeonyesha kuwa matumizi hayo ya muda mrefu husababisha matatizo ya kiafya, kama maumivu ya shingo (hasa kwa kuangalia simu au kucheza michezo ya kompyuta kwa muda mrefu). Pia husababisha maumivu ya kwenye mabega, mshtuko wa mishipa, na hata badae kusababisha maumivu ya uti wa mgongo.

4. Kutopata usingizi wa kutosha

Wakfu wa kulala wa Taifa umependekeza kuwa ili mtu wa makamo apate afya anatakiwa kulala kati ya masaa saba mpaka tisa kwa usiku.

Kwa bahati mbaya Wamarekani milioni 40 wanashindwa kutimiza kigezo hiko kutokana na kubanwa na ratiba za shughuli za kila siku. Kushindwa kulala usingizi wa afya kunaweza kuathiri maendeleo ya mishipa.

Utafiti uliofanywa katika huo Kikuu cha Uppsala kilichopo nchini Uswidi kimeonyesha kuwa kitendo cha kutolala kwa muda unaotakiwa kunaweza kuzalisha molekuli zinazoleta madhara ya ubongo.

5. Usingizi wa mchana

Baada ya kuangalia madhara yanayosababishwa kutokana na ukosefu wa usingizi, sasa tuangalie athari za kulala kwa muda mrefu.

Usingizi wa mchana unaweza kukusaidia kufanya shuhuli zako za kila siku, ila ukilala sana mchana pia kunaweza kuathiri shuguli zako.

Wataalamu wanashauri kuwa mtu anapaswa kulala mchana kwa dakika 30 tu (nusu saa tu). Maelezo ya taarifa ya utafiti kutoka European Prospective Into Cancer (EPIC)-Norfolk kimeonyesha kwamba watu wanaolala zaidi za saa moja mchana hujiongezea hatari ya kufa mapema mara 32.

6. Unywaji wa vinywaji laini (Soda)

Kwenye nukta hii, wote tunapaswa kujua ulaji wa afya ni ule usiosindikizwa na soda. Baadhi wanaweza wasitambue kiwango cha madhara kwenye afya zao kutokana na athari ya vinywaji laini vyenye sukari.

Kwa mfano, watu wanaokunywa soda moja kwa siku wako katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo (Heart Attack) kwa asilimia 20, hii imetokana na utafiti uliofanywa cha Chuo Kikuu cha Harvard.

Kiwango cha sukari kwenye soda ni sawa na vijiko 10 vya chai.
Maradhi mengine yanayosababishwa na unywaji soda ni kisukari, jongo (gout) na mengine zaidi. Ulionyesha utafiti huo.

Source:Yahoo News.
 
Top