dawa za uvimbe kwenye kizazi
Dawa mbadala 16 zinazotibu uvimbe kwenye kizazi (Fibroids) haraka
Uvimbe katika mfuko wa kizazi wa mwanamke hujulikana kama ‘uterine myoma’ au fibroid. Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi. Uvimbe huu hutokea katika sehemu mbalimbali juu au ndani ya mji wa uzazi wa mwanamke. Ni uvimbe ambao hauhusiani na kansa na unaweza kubadilika rangi ukawa wa njano, unaweza kubadilika ukawa kama maji tu na kurudi tena kuwa mgumu.
Uvimbe kwenye kizazi hujulikana pia kwa majina haya kitaalamu: ‘Uterine fibroids’, ‘Myoma’ au ‘fibromyoma’. Hujulikana pia kama ‘leiomyoma’ katika lugha ya kidaktari. Wanawake wenye umri kati ya miaka 30 hadi 50 ndiyo wanapatwa kirahisi zaidi na ugonjwa huu.
Chanzo cha moja kwa moja cha ugonjwa huu bado hakijulikani wazi, hata hivyo baadhi ya sababu za kutokea huu uvimbe ni pamoja na;
  • Kuongezeka sana vichocheo vya progesterone na estrogen kuzidi kiwango mwilini
  • Ujauzito
  • Uzito na unene kupita kiasi
  • Jenetiki zisizo za kawaida
  • Mfumo usio sawa wa mishipa ya damu
  • Sababu za kurithi
  • Lishe isiyo sawa
  • Sumu na taka mbalimbali nk
Dalili zitakazokuonyesha una uvimbe kwenye kizazi ni pamoja na;
  • Kupata damu nyingi wakati wa hedhi
  • Maumivu makala wakati wa siku za hedhi
  • Kuvimba miguu
  • Unaweza kuhisi una ujauzito
  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Kuhisi kuvimbiwa
  • Kupata haja ndogo kwa taabu
  • Kutokwa na uchafu ukeni
  • Kupata choo kigumu au kufunga choo
  • Maumivu nyuma ya mgongo
  • Maumivu katika miguu ikiwa ni pamoja na miguu kuwaka moto
  • Upungufu wa damu
  • Maumivu ya kichwa
  • Uzazi wa shida
  • Kutopata ujauzito
  • Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo
  • Maumivu ya nyonga
  • Mimba kutoka mara kwa mara (miscarriage)

Aina za Uvimbe kwenye kizazi
Kuna aina kuu nne za Fibroids
  • Intramural: Hutokea kwenye kuta za mji wa mimba (uterus). Wanawake wengi hupatwa na aina hii ya uvimbe.
  • Subserosal fibroids: Hii hukua nje ya kuta za mji wa mimba na hukua na kuwa kubwa sana.
  • Submucosal fibroids: Hutokea kwenye misuli chini ya ngozi laini ya kuta za mji wa uzazi.
  • Cervical fibroids: Hii hujenga kwenye shingo ya tumbo la uzazi (Cervix).

Dawa mbadala 16 zinazotibu uvimbe kwenye kizazi.
Ikiwa mwanamke hapati shida ya namna yo yote katika shughuli zake za kila siku, anaweza asihitaji tiba ya aina yo yote hata kama imegundulika kuwa ana uvimbe wa fibroid. Hii ni kutokana na ukweli kuwa  mwanamke anapokaribia kukoma hedhi Uvimbe huu hunyauka wenyewe na mara nyingine kutoweka kabisa.
Ikitokea kwamba  tiba imekuwa ni ya lazima, anaweza kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji kutokana na hali ilivyo.
Chagua dawa tatu hata nne kati ya hzi na utumie kwa pamoja kwa matokeo mazuri na ya haraka. Tafadhari usitumie dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa daktari, mganga au mtaalamu wako wa afya
  1. Kitunguu swaumu
Kitunguu swaumu ni chanzo kizuri cha vitamini B6, vitamini C, na madini mengine mhimu ambayo husaidia kuweka sawa homoni za kike. Sifa yake ya kuondoa sumu mwilini husaidia kuondoa uvimbe kwenye kizazi. Kitunguu swaumu pia huzuia kujitokeza kwa uvimbe wa aina yoyote kwenye mji wa mimba  (uterus).  Tafuna punje 3 za kitunguu swaumu kutwa mara 3. Kunywa maji glasi moja kila ukimaliza kutafuna kitunguu swaumu kuondoa ukali na harufu mbaya mdomoni.
  1. Juisi ya Limau
Moja kati ya dawa nyingine za asili kwa kuondoa uvimbe kwenye kizazi ni juisi ya limau. Ongeza vijiko vijiko vya juisi (majimaji) ya limau na kijiko kidogo cha unga wa baking soda kwenye glasi ya maji ya uvuguvugu, koroga vizuri na unywe mara mbili kwa siku kwa majuma kadhaa.

  1. Tangawizi
Mizizi ya tangawizi ni mizuri sana katika kupunguza maumivu na kuongeza msukumo wa damu. Andaa chai ya tangawizi (kumbuka ni tangawizi na maji tu, usiweke majani ya chai humo) na unywe kikombe kimoja kutwa mara 3 kwa majuma kadhaa. Kwenye hiyo chai tumia asli badala ya sukari kwa matokeo mazuri zaidi. Chai ya tangawizi husaidia kuondoa uvimbe kwenye mirija ya uzazi na kwenye mji wa uzazi kwa ujumla.
  1. Mafuta ya zeituni
Moja ya tiba za asili kwa uvimbe kwenye kizazi ni mafuta ya zeituni. Mafuta haya huidhibitihomoni ya  estrogen. Unahitaji kunywa kijiko kikubwa kimoja cha  mafuta ya zeituni sambamaba na juisi ya limau asubuhi mapema tumbo likiwa bado tupu. Unaweza pia kuandaa  mafuta ya zeituni kwa kuyapika majani ya mzeituni kama chai ambayo pia husaidia kuongeza kinga ya mwili.
  1. Mafuta ya nyonyo
Mafuta ya nyonyo ni mazuri sana kwa kuondoa uvimbe. Weka mafuta ya uvuguvugu ya zeituni kwenye bakuli. Weka kitambaa cha pamba ndani ya hayo mafuta mpaka mafuta yote yanyonywe na yahamie kwenye hicho kitambaa. Kunja kunja hicho kitambaa na uweke juu ya tumbo ndani ya mfuko wa Rambo na kisha weka chupa yenye maji ya moto juu yake (ilaze) na uache hivyo kwa usiku mmoja.  Endelea na zoezi hili kwa kila siku kwa siku 5 hivi kisha pumzika kwa siku mbili, rudia hivyo hivyo siku tano kisha siku mbili kupumzika. Ili kuyaona mabadiliko jaribu njia hii kwa wiki tatu hivi.

  1. Siki ya tufaa
Katika kutibu uvimbe wowote ambao si uvimbe wa kansa, siki ya tufaa ndiyo namba moja. Unachotakiwa kufanya ni kuchukuwa vijiko viwili vikubwa vya siki ya tufaa na uchanganye na maji glasi moja (robo lita/ml 250) changanya vizuri na unywe. Fanya hivi kutwa mara moja kwa majuma kadhaa.
Unaweza pia kuchanganya kijiko kimoja cha chai cha baking soda na vijiko viwili vya chai vya siki ya tufaa ndani ya glasi moja ya maji, tikisa vizuri mchanganyiko huo na unywe.
Mhimu – Kamwe usinywe siki ya tufaa ambayo haijapunguzwa makali (kavu kavu) yaani bila kuongezwa maji kidogo.

  1. Maziwa
Maziwa yanasaidia kuondoa uvimbe vizuri kabisa. Maziwa huwa na protini ya kutosha. Kwenye glasi moja ya maziwa ya uvuguvugu ongeza kijiko kimoja cha unga wa giligilani (coriander powder) na kijiko kimoja kikubwa cha unga wa binzari. Tikisa vizuri mchanganyiko huo na unywe yote. Fanya hivi kutwa mara 2 kwa wiki kadhaa.

  1. Unga wa Binzari (manjano)
Sifa ya kimatibabu iliyomo kwenye binzari hupigana pia dhidi ya uvimbe kwenye kizazi. Chukua vijiko vikubwa viwili vya unga wa binzari au unga wa mizizi yake na changanya na maji nusu lita, chemsha kama chai kwenye moto kwa dakika 15, ipua na uache kwa dakika 40. Ikipoa kunywa yote. Fanya hivi kwa wiki kadhaa.
  1. Kitunguu maji
Viuaji sumu (antioxidants) vilivyomo kwenye kitunguu husaidia kuondoa uvimbe kwenye kizazi kirahisi zaidi. Kitunguu pia ni mhimu katika kurekebisha na kuweka sawa homoni za kike. Kwahiyo kupunguza uvimbe anza sasa kutafuna kitunguu maji kibichi kama kilivyo, usikioshe na chumviwala maji. Kata nusu kitunguu maji na ule kama kilivyo kila siku kwa wiki kadhaa uvimbe utaondoka na homoni zako zitakaa sawa.

  1. Zabibubata (Gooseberry)
Zabibubata ni moja ya dawa mbadala zinazotumika sana dhidi ya matatizo mengi ya ngozi na nywele kwa ujumla. Changanya unga wa zabibubata kijiko kidogo cha chai kimoja na kijiko kidogo kingine cha asali. Changanya vizuri mchanganyiko huo na ulambe wote. Inashauriwa kutumia dawa hii asubuhi mapema wakati tumbo likiwa tupu.
Ni dawa nzuri sana katika kupunguza ukubwa wa uvimbe wa kwenye kizazi (fibroid tumors).

  1. Maharage ya soya (soybeans)
Ili kuondoa dalili za uvimbe kwenye kizazi kula maharage ya soya mara nyingi. Maharage ya soya yana kiinilishe mhimu sana kijulikanacho kama “phytoestrogen” ambacho husaidia kudhibiti usawa wa homoni ya kike ‘estrogen’. Andaa supu au mchuzi wa maharage ya soya, protini iliyomo kwenye maharage ya soya huzuia kuendelea kukua au kuongezeka kwa uvimbe kwenye kizazi.

  1. Yoga na Meditation
Moja ya njia rahisi kabisa ya kuondoa uvimbe kwenye kizazi na kufanya mazoezi maalumu yajulikanayo kama YOGA. Yoga ni sayansi ya kimatibabu yenye asili ya India na ina zaidi ya mika 5000 tangu ilipoanza kutumika. Haya ni mazoezi maalumu yanayoambatana na utulivu wa nafsi ikihusisha mambo ya kiroho. Kuelewa namna hasa mazoezi haya yanavyofanyika ona video zake kwenye youtube kwa kubonyeza hapa => https://goo.gl/TiKHZd .
Meditation ni kama Yoga lakini unapomeditate maana yake unajiondoa kwenye mazingira ya kawaida na kubaki peke yako kwa masaa kadhaa katika hali ya utulivu, kama ni kazi unaacha, unaacha pia kukaa na vitu kama simu, computer au kuwa tu karibu na yeyote. Hii ni mhimu kwa mtu yeyote anayehitaji kuondoa msongo wa mawazo na kuungezea nguvu ubongo upya.  Yoga na meditation (utulivu) husaidia kuweka sawa mzunguko wa hedhi na hata kuziweka sawa homoni zako.
  1. Samaki
Samakai wana mafuta mhimu sana mwilini yajulikanayo kama omega-3 fatty acid ambayo ni mhimu sana katika kutibu uvimbe kwenye kizazi. Unahitaji kutumia mara kwa mara samaki wa maji baridi kama samoni (salmon), jodari ( tuna), na samaki wengine wenye minofu wa maji baridi ili kuondoa uvimbe.

  1. Asali
Ili kuondoa uvimbe maji katika mirija ya uzazi, asali inaweza kuwa msaada mkubwa kwa kazi hiyo.  Changanya juisi ya aloe vera, asali na maji na unywe mchanganyiko huu. Chukua glasi moja ya maji, ongeza kijiko kidogo kimoja cha asali mbichi na kijiko kikubwa kimoja cha juisi ya mshubiri (fresh aloe vera jusi), tikisa vizuri na unywe mchanganyiko huu.

  1. Kiazi sukari (beet) na kitunguu swaumu
Ili kuandaa juisi ya kuondoa uvimbe, saga kiasi kidogo cha viazi sukari freshi  na uchanganye pamoja na kijiko kidogo cha chai kimoja cha unga wa kitunguu swaumu. Changanya mchanganyiko huo vizuri na uongeze kikombe kimoja cha juisi freshi ya karoti, ongeza kijiko kimoja kidogo cha asali, tikisa vizuri na unywe mchanganyiko huu mara kwa mara mpaka utakapopona.

  1. Aloe Vera (mshubiri)
Moja kati ya mimea kwa ajili kutibu maradhi mengi katika mwili wa binadamu ni aloe vera au mshubiri kwa kiswahili. Aloe vera pia hutibu uvimbe wa kwenye kizazi bila shida yoyote. Unachohitaji ni kuchanganya ¼ ya kikombe cha juisi ya aloe vera na kikombe kimoja juisi ya viazi sukari (beet) katika glasi moja. Ongeza kiasi kidogo cha juisi ya limau na jaza maji ya kutosha kujaza vizuri hiyo glasi. Kunywa glasi moja kutwa mara 1 kwa wiki kadhaa ili kuondoa uvimbe katika kizazi.
Tafadhari Zingatia haya kuwezesha uvimbe kupona haraka
  • Hakikisha una uzito sawa kila mara kulingana na urefu wako.
  • Kula sana mboga za kijani na matunda
  • Fanya mazoezi ya viungo kila mara, mara 4 mapaka 5 kwa wiki
  • Kunywa maji mengi kila siku lita mbili mpaka lita tatu
  • Kula sana vyakula vyenye nyuzi nyuzi (faiba) na punguza vyakula vyenye mafuta
  • Usitumie bidhaa zozote zenye kaffeina (chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi zote nk), nyama nyekundu na vyakula vya kuchomwa au kupikwa katikati ya mafuta mengi (maandazi, chipsi, nk)
  • Achana kabisa na mawazo mawazo (stress) na hamaki nyingine zozote
  • Acha kuvuta sigara/tumbaku na vilevi vingine vyote hadi hapo utakapopona kabisa
Ikiwa utahitaji dawa za uvimbe kwenye kizazi zilizokwisha kuandaliwa tayari kwa mfumo wa virutubisho bila kemikali nitafute kwenye 0625539100
 
Top