Matumizi ya chupa za chuchu za mpira (bottle feeding) kwa matumizi ya watoto ni nzuri zinarahisisha mtoto kunywa kwa urahisi ila ni hatari kwa afya ya mtoto,iwapo mzazi hatozingatia usafi basi mtoto anahatari ya kupata maradhi kama kuhara,infection au maumivu makali ya tumbo.
Chupa kawaida inatabia ya kutengeneza uterezi kwa ndani ikiwa haisafishwi kwa brush lake kwa kusugua ndani,uterezi huo unakuja kuzalisha bacteria watakao mshambulia mtoto akiwa anakunywa maji,juice au maziwa n.k
Chupa za plastic zinazo tengenezwa kwa kutumia material ya bisphenol sio nzuri kwa afya ya mtoto baada ya kufanyiwa tafiti mwaka 2012 wakashauri zisitumike na nivizuri mzazi akasoma maelezo ya chupa kabla ajanunua. Chupa zenye material ya glass ni nzuri zaidi kwa matumizi ya mtoto hata kupashia maziwa haina tatizo kama ya plastic ni rahisi kuyeyuka na sumu kuingia kwenye maziwa.
HIZI NI CHUPA ZA TOMMEE TIPPEE ZINASIFIKA KWA UBORA KAMA ZA AVANT ZOTE NI NZURI JAPO NI GHARAMA ZA JUU
Vituo vingi vya afya hawashauri wazazi kutumia chupa za watoto sababu wengi wanashindwa kuzisafisha vizuri na kupelekea watoto kupata maradhi.Kuna aina nyingi za chupa ila mimi ninapendelea chupa za Avant zina ubora mzuri kwa materials wanazotumia na wanachombo special cha kusafishia chupa zao(steam sterilizer)
Mtoto afunzwe kutumia kikombe mapema akiwa na miezi 6 itamsaidia zaidi na kujiepusha na maradhi
Jinsi ya kusafisha chupa ya mtoto
Tumia brush la kuoshe chupa ambalo utasugulia mule ndani kutoa uterezi ,chuchu ibidue geuza ndani nje nje ndani nayo usafishe utaosha kwa maji safi baada ya hapo fungua chupa kwa tenganisha mifuniko,chupa, chuchu na ile ring yake ya kukazia chupa wakati wa kufunga .
BRUSH ZA KUOSHEA CHUPA IZO NDEFU NI ZA CHUPA,IZO FUPI NDOGO NI ZA CHUCHU KULE MBELE NDANI MTOTO ANAPO NYONYEA
Bandika sufuria jikoni weka maji ya kutosha dumbukiza chupa na uache zichemkie kwa dakika 5-10 ili kuuwa vijidudu ,baada ya hizo dakika epua mwaga maji baada ya kuosha chukua kitambaa safi cha vyombo ,tandika sehemu safi na kavu mfano kwenye meza weka chupa zake geuza juu chini ili maji yatoke na zibaki imekauka.
Kuna kifaa kinaitwa Steam sterilizer cha kuchemshia chupa za watoto nazo ni zuri zinasafisha vizuri na kuuwa bacteria
Ushauri wa afyaborakwamtoto
Mama hakikisha hili zoezi unalifanya mwenyewe kuosha chupa kiufasa kabsa, kama unamwachia dada wa nyumbani kusafisha hakikisha umemfunza vizuri .Nunua chupa ziwe zaidia ya 3 itamsaidia mtoto kubadili kwa urahisi tofauti na akiwa na moja hiyo hiyo ni ngumu kuoshwa kwa kila mara baada ya kutumika na nunua chupa za glass iwapo ukapo nunua ya plastic usinunue yenye (bisphenol A) iyo ni sumu mbaya kwa mtoto.