aflatoxin2
Sumu kuvu inayojulikana kitaalamu kama mycotoxins(Mycotoxin ni jina la jumla. Aina maalum za mycotoxin zinahusishwa na aina tofauti za kuvu, kama vile aflatoxins na Aspergillus). Aina zote mbili za kuvu (aflatoxins na Aspergillus) pia huzalisha mycotoxins nyingine, ni aina za kemikali za sumu zinazozalishwa na aina ya ukungu au fangasi wanaoota kwenye mbegu za nafaka kama vile mahindi, mbegu za mafuta kama karanga, jamii ya kunde, mazao ya mizizi na pia vyakula na malisho ya wanyama.Sumu kuvu pia hupatikana katika bidhaa za mifugo kama vile maziwa, mayai na nyama pale ambapo chakula kinacholiwa na mifugo kitakuwa kimechafuliwa na sumu hizo.Vilevile baadhi ya sumu kuvu hupatikana kwenye maziwa ya mama anayenyonyesha iwapo atakula chakula kilichochafuliwa na sumu hizo.Ingawa kuna aina nyingi za fangasi ambao wanaweza kuota na kukua katika vyakula hivi, ni fangasi wachache tu ambao hutoa sumu kuvu.Sumu kuvu haiwezi kuonekana kwa macho, haina harufu, haina kionjo na wala haina rangi. Ukungu unaotokana na sumu kuvu unaweza kuwa na rangi ya kijani, chungwa, kijivu, au njano chafu na unaweza kutoa harufu ya uvundo.Ukungu huo unaotoa sumu kuvu, hustawi ikiwa mazao yamekumbwa na ukame yakiwa shambani au kushambuliwa na wadudu waharibifu na yakahifadhiwa kwenye ghala lenye joto na unyevu katika kiwango cha juu.
MADHARA
Uharibifu unaosababishwa na Aspergillus na Fusarium kwa mimea iliyosimama ni mdogo ukilinganishwa na athari
mbaya ya afya ya binadamu na mifugo kutokana na kumeza mycotoxins. Madhara kwa watoto wadogo na wakati wa
ujauzito ni mabaya zaidi. Kuku wako hatarini zaidi ya kuathiriwa na mycotoxins.
Mycotoxins haziwezi kuonekana na hazina harufu, ladha au rangi na zinaweza tu kuonekana kupitia uchambuzi wa
kikemikali. Uwepo wake mara nyingi tu hudhihirika kutokana na dalili zinazoonekana kwa watu na wanyama ambao
walikula bidhaa za mahindi zilizosibikwa, hasa katika kipindi cha muda mrefu. Kula mycotoxin kwa muda mrefu (sugu)
husababisha kupungua kwa kinga dhidi ya magonjwa, uharibifu wa figo na ini, na watoto hudumaa.
Makadirio ya kuaminika yanaonyesha kwamba asilimia 25 ya chakula duniani kina mycotoxins na kwamba watu bilioni
2.5 mara kwa mara wanazila. Idadi kubwa ya udongo (asilimia 40-80) ina aina za Aspergillus zinazotoa aflatoxin. Hasara
ya kifedha ni kubwa. Kupungua kwa mauzo ya nje ya njugu kutoka Afrika (ili kufuata mahitaji ya Jumuia ya Ulaya ya
vipimo vya mycotoxin) kulimaanisha hasara ya kila mwaka ya dola milioni 670 za Marekani kwa nchi za kuuza njugu nje.
Mfano wa madahara yanayosababishwa na ulaji wa kuvu aina ya aflatoxin ni mlipuko wa ugonjwa ulioripotiwa huko Kondoa, Dodoma, kama ambavyo waziri wa Afya alivyonukuliwa na vyombo vya habari akiongelea mlipuko wa ugonjwa huo,“Waziri wa Afya alisema hadi sasa ni sampuli za nafaka pekee, zilizofanyiwa uchunguzi zilizoonyesha kuwapo kwa sumukuvu (aflatoxins).“Jumla ya sampuli 13 kati ya 27 zilikuwa na uchafuzi wa sumukuvu kwa kiasi kisicho kubalika kwenye nafaka kwa mujibu wa viwango vya kitaifa na zote zilibainika kwenye mahindi. Sampuli 12 zilitoka Chemba, moja Kondoa,” alisema waziri huyo.
Acute exposure (kula sumu nyingi kwa wakati mmoja) ndio inaweza kusababisha madhara ya vifo vya ghafla kama ilivyotokea Dodoma. Hata hivyo chronic exposure (kula vyakula vyenye kiwango kisichoua papo kwa hapo, kwa muda wa miaka mingi) ndio tatizo kubwa zaidi kwani hupelekea madhara mengi kama saratani ya ini, kudumaa mwili na akili, udhaifu wa kinga mwilini na kadhalika.
KUJIKINGA
Njia za kudhibiti maambukizi ya sumu kuvu
Kuna njia mbalimbali ambazo mkulima anaweza kuzitumia ili kupunguza uchafuzi wa sumu kuvu katika mazao yake yakiwa shambani au baada ya kuvuna. Njia hizo ni kama zifuatazo;
• Lima aina za mazao yenye ukinzani dhidi ya kuvu wanaotoa sumu kuvu (kama inapatikana).
• Vuna mazao yakiwa yamekauka vizuri kama inavyoshauriwa na afisa wa kilimo na pia epuka kutia majeraha katika mazao yako.
• Usianike mazao yako kwenye udongo mtupu. Tumia turubai au aina nyingine ya vifaa vya kuanikia au kukaushia mazao
• Wakati na baada ya kuvuna chambua na kuondoa mbegu zilizooza, zilizovunjika, zilizotobolewa au kuharibiwa na wadudu pamoja na zile zilizobadilika rangi.
• Hifadhi mazao mahali pakavu na pasipo na joto. Hakikisha mazao yaliyohifadhiwa hayanyeshewi na mvua au kulowa maji.
• Hifadhi mazao kwenye ghala linaloruhusu mzunguko wa hewa.
• Zuia wadudu waharibifu na kuvu kwa kunyunyiza madawa yaliyokubalika na kushauriwa na wataalamu wa kilimo.
• Unaweza pia ukakoboa mahindi na kuchambua vizuri kabla kuyahifadhi ili kuondoa yale yanayoelekea kuwa na uchafuzi wa sumu kuvu ambayo huwa zimeanza kubadili rangi.
• Kama yanapatikana, tumia madawa ya kibayolojia kama vile Aflasafe (aina ya kuvu ambaye hukinzana na yule anayetoa sumu kuvu).
• Tumia madawa yaliyodhibitishwa kuondoa sumu kuvu wakati wa usindikaji (utengenezaji) wa vyakula vya binadamu na vile vya wanyama.
 
Top