Ni ugonjwa wa aina gani?
Hepatitis B ni virusi vinavyoenea katika ini na kusababisha
madhara makubwa katika ini. Ini ni muhimu mwilini na kazi
yake ni kusaga vyakula pamoja na kemikali zinazoleta madhara,
kutengeneza protini na kuhifadhi vitamini muhimu, madini, na
sukari.
Dalili zake ni zipi?
Idadi kubwa ya watu wenye hepatitis B hawajijui kama
wameambukizwa kwa sababu hawaonyeshi dalili zozote. Watu
wengine wanaweza kuwa na dalili kadhaa wanapoambukizwa
kwa mara ya kwanza. Wanaweza kuwa na aina fulani ya mafua,
kuwa na uchovu sana, kukosa hamu ya kula, ngozi na macho
kubadilika rangi ya njano (homa ya manjano); na/au mkojo
mweusi. Yoyote mwenye ugonjwa huu anaweza kuambukiza
watu wengine, hata kama hana dalili yoyote au hata kama hajui
kama anaumwa. Njia pekee ya kujua kama umeambukizwa na
Hepatitis B ni kupima damu ili kugundua uambukizo.
Maelezo zaidi kuhusu hepatitis BIdadi kubwa ya wagonjwa watu wazima huwa wanapata nafuu
ya ugonjwa huu. Ijapokuwa, kati ya watu 100 wenye ugonjwa
huu:
• mtu 1 anaweza kuwa na madhara makali yanayosababisha
maini yasifanye kazi vizuri mara baada ya kuambukizwa; na
• watu kama 5 wataendelea kuwa na ugonjwa huu kwa
muda mrefu – watakuwa wabebaji wa virusi na wanaweza
kuambukiza watu wengine. Angalau mbebaji 1 atapata madhara
makali ya ugonjwa wa ini maishani.
Watoto na watoto wachanga walioambukizwa ugonjwa huu wa
hepatitis B wana uwezo mkubwa wa kuwa wabebaji wa virusi,
ijapokuwa ukiwalinganisha na watu wazima, watoto wana
uwezo mdogo wa kuonyesha dalili zozote za ugonjwa. Mara
nyingi mtoto mgonjwa anakuwa na virusi hivi mwilini kwa
muda mrefu wa maisha yake na kuna uwezo mkubwa wa
kuwekeza ugonjwa huu mwilini na kuja kupata saratani ya ini baadae.
Tiba
Tiba ya hepatitis B bado haijapatikana ingawa kuna matibabu
ambayo yanaweza kusaidia ini lisiendelee kuharibika na virusi
visiendelee kuzaliana. Mafanikio ya chanjo yanatofautiana kati
ya watu tofauti.
Kuna aina zingine za magonjwa ya hepatitis, kama vile hepatitis
A na hepatitis C, ambayo ni tofauti na hepatitis B.
Unapataje ambukizo la ugonjwa huu?
Hepatitis B ni virusi vilivyopo katika damu na katika majimaji
ya miili ya wagonjwa. Ni ugonjwa unaosambaratika kirahisi.
Huambukizwa kwa njia ya kujamiiana kati ya mtu mwenye
uambukizo na asiyenao kwa njia ya:
• kujamiiana na mtu mwenye uambukizo bila kutumia
kondomu (ngono kati ya mwanamke/mwanamme na
mwanamme/mwanamme). Hii ni hatari kwa sababu majimaji ya
mwili yanaweza kuwa na virusi;
• kutoka kwa mama mgonjwa hadi kwa mtoto wake;
• kuchangia vifaa vya kujitunga madawa ya kulevya (kama
vile sindano, vijiko, maji na vichujio);
• kuchangia miswaki, mashine ya kunyolea au vifaa vya
kuchorea mwili na vya kutoboa ngozi visivyotakaswa vizuri; au
• kuongezewa damu (kwa mfano kupokea damu
iliyoambukizwa na virusi au vifaa vya damu).
Nani yuko katika hatari ya kuambukizwa?
Watu walioko katika vikundi vifuatavyo wanaweza kuwa katika
hatari ya kuambukizwa na hepatitis B:
• watoto wanaozaliwa na mama mwenye uambukizo;
• mwenza, mtoto, au mtu anayeishi nyumbani mwenye
uambukizo;
• watu wanaofanya kazi katika sehemu ambazo wanaweza
kushika majimaji ya mwili, kwa mfano madaktari, manesi,
daktari wa meno, maafisa wa magereza, au polisi;
• mtu anayefanya mapenzi na watu tofauti mara kwa mara,
haswa wale ambao hawatumi kondomu; au
• mtu anayejidunga sindano ya madawa ya kulevya na
kuchangia vifaa vya kujidunga madawa.
Kama unafikiri wewe, au mtu yoyote katika familia yako,
anaweza kuwa hatarini ni vizuri kuonana na wataalamu wa afya kwa ushauri zaidi.
Naweza kujikinga na ugonjwa wa hepatitis B?
Ndio. Kuna chanjo nzuri sana inayopatikana. Kama unafikiri
uko katika hatari kubwa ya kupata hepatitis B ongea na wataalamu wa afya. Wao watakusaidia kuamua kama kuna haja ya wewe kuchanjwa ili uwe na kinga na pia wanaweza kukupa ushauri wa
kupunguza hatari ya uambukizo.
Chanjo ya Hepatitis B ni chanjo ambayo kwa kawaida hutolewa kama dozi
ya chanjo 3. Chanjo hii ni salama na nchi nyingi duniani
zinaitumia ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa kuchanja watoto.
Ni jambo la muhimu sana kumaliza dozi yote ili ifanye kazi
yake vizuri.
 
Top